DC MTEULE ATAKIWA KUKOMESHA MAUAJI WILAYANI NZEGA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 14, 2020

DC MTEULE ATAKIWA KUKOMESHA MAUAJI WILAYANI NZEGA


 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (kulia) akimwapisha Mkuu wa Wilaya ya Nzega Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Advera Bulimba (kushoto) baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuongoza Wilaya hiyo.
 Baadhi ya viongozi wakiwa katika Halfa fupi ya kuapishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega Advera  Bulimba baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuongoza Wilaya hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega    Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Advera Bulimba (mbele) na Wakuu wa Wilaya nyingine za Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (hayupo katika Picha) wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Nzega jana.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati akiwahutubia viongozi mbalimbali mada baada ya kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Nzega  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Advera Bulimba aliyeteuliwa hivi karibini  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuongoza Wilaya hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega    Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Advera Bulimba akizungumza mara baada ya kuapishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati(hayupo katika picha)

 Mkuu wa Wilaya ya Nzega    Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Advera Bulimba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati(katikati) na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kushoto) mara baada ya kuapishwa jana.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega    Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Advera Bulimba (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati(wa tatu kutoka kushoto) , Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama( kushoto) , Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya( wa pili kutoka kushoto) , Mkuu wa Wilaya ya Igunga wa pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala (kulia) mara baada ya kuapishwa jana.Picha na Tiganya VincentNA TIGANYA VINCENT, TABORA.

MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Nzega Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera Bulimba kuhakikisha anakomesha vitendo vya mauaji vinavyotokana na wananchi kujichukulia Sheria mikononi.

Ametoa agizo hilo jana mara baada ya kumuapisha Mkuu huyo mpya wa Wilaya ya Nzega anayekwenda kushika nafasi ya Godfley Ngupula.

Alisema Wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo la baadhi wa watu kuamua kuwaua wenzao kwa imani za kishirikina na wivu wa kimapenzi , jambo linalotia doa Mkoa.

“Nenda ukatumie ukatumie uzoefu wako na mafunzo na ujuzi ulionao ukakomesha tabia ya baadhi ya watu kuamua kukatisha maisha ya wenzao…mkashirikiane na viongozi wenzao kuhakikisha tatizo hilo linakwisha na wananchi wote wanaishi kwa Amani”alisema.

Alisema ni vema wakahakikisha wanasimamia haki na kufanyakazi kwa usawa ili wanyonge wanoanyanyaswa wapate kilimbilio na kupata majawabu ya kero zao ili Wilaya hiyo iwe mfano kwa Mkoa wa Tabora.

Dkt. Sengati alimtaka kuhakikisha anasimamia watumishi waliochini yake katika kujenga uchumi wa Wilaya ya Nzega na kuimarisha upatikanaji huduma bora kwa wananchi hasa kwa wale wanaoishi pembezeni.

“Nenda ukachape kazi ili uweze kuacha alama kama kielelezo cha utendaji wake kwa wananchi” alisema

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliwataka vijana walioteliwa kushika nafasi mbalimbali kuhakikisha wanafanyakazi kwa uzalendo na uadilifu ili kumwonyesha Mhe. Rais kuwa hakukosea kuwaamini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nzega Kamishina Msaidizi wa polisi Bulimba alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumwamini na kuweza kumteua kushika nafasi hiyo ya uongozi.

Aliahidi kuchapa kazi ya kuwatumikia wananchi kwa haki na usawa bila ya upendeleo ili kumwakilisha Rais ipasavyo katika Wilaya hiyo.

ACP Bulimba aliwataka kushirikiana katika kuhakikisha wanatatua matatizo ya wananchi ili waweze kufikia malengo yao.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Nzega aliteuliwa hivi karibuni kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Godfrey Ngupula ambaye amestaafu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad