DAWASA yawatua ndoo wakazi wa King'azi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 23, 2020

DAWASA yawatua ndoo wakazi wa King'azi

Wakazi wa Mtaa wa King'azi "A" na "B" wameishukuru Serikali kwa kupata huduma ya Maji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), wakazi hao wamesema kulikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa Maji katika Mitaa hiyo kabla ya ujio wa Mradi huo wa Maji uliopo chini ya Halmashauri ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza walipotembelewa na Maafisa wa DAWASA kutokan Kitengo cha  kinachosimamia Miradi ya Maji pembezoni mwa Jiji (Offgrid) wameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Rais wake, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa utendaji kazi wake sambamba na Viongozi wake wa chini.

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Magufuli, kwa DAWASA kufanikisha huduma hii ya Maji, tulikuwa tunanunua Maji Ndoo kubwa Moja kwa Shilingi 500 na  tukiagiza Maji kwa Magari tunakaa wiki nzima baadae tunaletewa Maji kwa dumu la Lita 1000, tunalipa Shilingi 15000. Kwa kweli tunawashukuru sana DAWASA kwa kuleta huduma hii ya Maji hii ni moja  ya Kututua Ndoo akina Mama", amesema Halima Sheshe, Mkazi wa King'azi B.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maji King'azi B, John Joseph Lumatu ameishukuru Serikali kupitia DAWASA kufikisha huduma hiyo karibu na Wananchi wake, pia ameomba kwa DAWASA kuangalia sehemu nyingine kuendelea kutatua changamoto hizo za upatikanaji wa Maji.

"Hatukutegemea kama tunaweza kupata Maji kama hivi, nawashukuru viongozi wote, DAWASA kufanikisha kupata huduma ya Maji katika Mtaa wa King'azi, changamoto kubwa ilikuwa Kisima kilikuwa kinasimamiwa na Kamati ya Maji kule Juu baada ya ujio wa Mkuu wa Wilaya kuvunja Kamati hiyo, hivyo kukabidhiwa DAWASA hilo tunashukuru", amesema Lumatu.

Kwa upande wake, Afisa wa DAWASA, Kitengo cha kinachosimamia Miradi ya Maji pembezoni mwa Jiji (Offgrid), Mark Stanley amesema Mradi wa Mtaa wa King'azi A na B upo chini ya Halamashauri ya Ubungo hivyo wamefanya  maboresho ya mradi kuongeza vituo cha kuchotea maji nane wakati vituo vinne vipo King'azi B na vitatu mtaa wa King;azi A, Stanley amesema wataendelea kuboresha mradi huo ili lengo na  azma ya Serikali kutua Mama Ndoo Kichwani itimie.

Pia amesema kuna mchakato unafanyika ili kuhamisha mradi huo
chini ya Halamashauri ya Ubungo na kupelekwa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) ili kongeza ufanisi kwenye utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.
Mjumbe wa Serikali ya mtaa King'azi "B", Halima Twalib akimwagiwa maji na wakazi wa mtaa huo kwa kuonesha furaha mara baada ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA) kutoka kwa mara ya kwanza ikiwa ni jitihada za mjumbe huyo kufanikiwa upatikanaji wa maji katika Mtaa wa King'azi "B" kata ya Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam
Mwanyekiti wa Serikali ya mtaa King'azi "A", Juma said Msumali  akitolea ufafanuzi wa mradi wa maji ulioko chini ya Manispaa ya Ubungo ambapo uko kwenye mchakato wa kutolewa kwenye manispaa na kupewa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA) kwa ajili ya usambazaji katika mtaa wa Kwembe hasa kwenye mtaa wa King'azi "A" na "B".
Afisa wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA) kutoka kwenye kitengo kinachosimamia miradi ya maji pembezoni mwa jiji ( Offgrid) Mark Stanley akitoa ufafanuzi wa mradi wa maji wa King'azi "A" na "B" unaotakiwa kutoka Manispaa ya Ubungo na kwenda DAWASA wakati wa ziara ya kuhakikisha maji yanatoka katika vituo vilivyowekwa na DAWASA.
Mwenyekiti wa Kamati ya maji mtaa wa King'azi "B", John Joseph Lumatu(wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa maofisa wa DAWASA kuhusu namna walivyojipanga kama kamati ya maji ya mtaa ili kuhakikisha wananchi wa mtaa huo wanapata maji kwa wakati ili kuondoa hadha ya upatikanaji wa maji iliyokuwa inawakabili.
Afisa wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA) kutoka kwenye kitengo kinachosimamia miradi ya maji pembezoni mwa jiji ( Offgrid) Mark Stanley akitoa ufafanuzi kuhusu namna DAWASA ilivyojipanga katika usambazaji wa maji katika mitaa ya King'azi "A" na "B" ili kumtua mama ndoo kichwani.
Afisa wa Habari kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA), David Nkulila  akishuhudia wananchi wanavyochota maji ya DAWASA katika mtaa wa King'azi "B" ikiwa ni majaribio ya usambazaji wa maji katika mtaa huo na mitaa mingine katika kata ya Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Maofisa kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA) wakishuhudia utokaji wa maji kwa mara ya kwanza katika mtaa wa King'azi B kwenye mradi wa maji wa DAWASA uliokuwa katika Manispaa ya Ubungo wakati wa majaribio wa usambazaji wa maji katika kata ya ya Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Dawasa kutoka kwenye kitengo kinachosimamia miradi ya maji pembezoni mwa jiji ( Offgrid) Mark Stanley akitolea ufafanuzi moja ya kisima cha maji  kinachosambaza maji katika mtaa wa King'azi "B" kata ya ya Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad