Bado asilimia 60% ya kaya nchini Tanzania ndizo zinatumia madini Joto toshelevu - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 7 July 2020

Bado asilimia 60% ya kaya nchini Tanzania ndizo zinatumia madini Joto toshelevu

Mkurungezi mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe TFNC Dkt,Germana Leyna amesema hayo ni kwa mujibu wa kiwango cha kimataifa. Kuwa ili jamii isiwe na matatizo ya ambayo yanatokana na upungufu wa madini joto

Leyna amesisitiza kuwa jamii kuona umuhimu wa kutumia chumvi yenye madini joto ambayo ni tosheleza hasa watoto wadogo kwaajili ya ukuaji wa ubongo

“Toka mwaka 2015 kiwango cha kaya ambazo kinatumia chumvi yenye madini joto ya kutosha hakijaongezeka,kimebakia pale pale kwenye asilimia 60% kwa hiyo tumekuwa tukijaribu kutafuta ni sababu gani ambazo zinasababisha ni sababu gani ambazo zinasababisha idadi ya kawa ambazo zinatumia madini joto toshelevu”alisema Dkt,Germana Leyna

Anna John ni afisa lishe mwandamizi kutoka Taasisi ya chakula na lishe Tanzania amesema upungufu wa madini joto bado ni changamoto na huathiri watu wa makundi yote.

“Upungufu wa madini joto ni tatizo kubwa na tatizo hili huwaathiri sana watu wa makundi yote na kirubishi hiki cha madini joto kinapatikana ardhini ila kwasababu ya mafuriko na matatizo mengine ya mabadiliko ya tabia ya nchi utakuta kwenye ardhi tena kirutubisho hiki hakipatikani kwa urais.Kwa hiyo mwanadamu anaweza akapata madini joto kwa kula vyakula ambavyo vimepandwa kwenye ardhi yenye madini joto ya kutosha”alisema Anna John

Tanzania imetajwa kutopanda katika Kiwango cha kaya zinazotumia chumvi yenye madini joto ya kutosha na kuendelea kusalia na asilimia 60 kutoka mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020.

Hatahivyo, Kirutubishi cha madini joto kinapatikana ardhini lakini kutokana na mabadiliko ya tabia Nchi pamoja na mafuriko ambayo yanatokea yamechangia kuondoka na udongo wa juu wa madini joto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad