ShuleSoft inakuletea Rudi Shule na ShuleSoft - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 26 June 2020

ShuleSoft inakuletea Rudi Shule na ShuleSoft

Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Ephraim  Swilla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (June 26,2020) wakati akitambulisha kurudi shule na shuleSoft shule zinapokaribia kufungua. Kulia ni Afisa Masoko wa ShuleSoft, Christopher Anyimike.
 Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Ephraim Swilla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha wanafunzi, wamiliki wa shule pamoja na wazazi kurudi shule na shuleSoft ili kuendelea kutumia mifumo ya Kidijitali kujipatia elimu na kuendesha mifumo mbalimbali ya shule bila usumbufu.
Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Ephraim Swilla akitoa maelekezo jinsi mfumo wa shule soft unavyoweza kufanya kazi mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani.

TAASISI isiyo ya kiserikali ya mifumo ya Teknolojia ya elimu hapa nchini kupitia mtandao wa shulesoft ambao unaratibu shughuli za shule zote hapa nchini imekuja na kampeni mpya inayoitwa Rudishule na ShuleSoft. 

Lengo la kampeni hiyo ni kuhimiza wamiliki wa shule mbalimbali wasiendelee kutumia mifumo isiyo ya kidigitali katika kusimamia shughuli za shule na kutumia mifumo ya kidijitali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 26,2020, Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Ephraim Swilla amesema kuwa kwa kipindi hikia ambacho shule zinakwenda kufungua Juni, 29,2020 mfumo wa kidijitali wa ShuleSoft unaendelea kusaidia shule katika mambo kadhaa wa kadhaa ikiwemo kusimamia taaluma ya Shule kwa kuandaa ripoti za kisasa na zenye ubora, kurahisha makusanyo ya ada kupitia Control number.

Hata hivyo amesema kuwa mfumo huo utarahisha uandaaji wa mishahara kwa kuchakata taarifa za watumishi wote, kuandaa ripoti za kifedha kwa urahisi na ufanisi zaidi.

"Pia mfumo huu utasaidia kuboresha zaidi mawasiliano na wazazi ambapo wazazi hupata taarifa za shule kwa njia ya SMS, barua pepe, Telegram na pia kwa kuingia kwenye akaunti zao za ShuleSoft."

"Tunapo rudi shule, tunapenda kuwaambia wateja wetu kuwa ShuleSoft imeboreshwa sana sana na vipengele vipya vimeongezwa vinavyoleta ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wake, pamoja na kuhahikisha wamiliki na wasimamizi wa Shule wanapata faida katika kazi zao, na taaluma ya shule inasonga mbele." Amesema Swilla.

Hata hivyo Swilla amesema kuwa mfumo wao wa kidijitali umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mzazi anapata taarifa zote za mwanafunzi kupitia mfumo wa ShuleSoft popote alipo duniani.

Licha ya hilo amewakaribisha wamiliki wa shule kurudi shule na ShuleSoft kwa kuunganisha shule zao na mfumo mahiri wa ShuleSoft wenye gharama nafuu sana.

Mfumo wa shuleSoft uliweza kusaidia wanafunzi wa shule mbalimbali katika kipindi shule zilipokuwa zimefungwa kutokana na ugonjwa wa Corona (Covid-19) kwa kuwa na walimu wanaofundisha masomo mbalimbali katika mtandao huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad