HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 27, 2020

BASHUNGWA ATANGAZA UKOMO WA BEI ZA BARAKOA, AELEKEZA VIWANDA VYA NGUO NCHINIKUTENGENEZA BARAKOA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amesema atachukua hatua kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazouza barakoa kwa gharama kubwa.


Bashungwa alitoa taadhari hiyo mkoani Arusha alipotembelea Viwanda vya kuzalisha nguo vya Sunflug na A to Z kuangalia hali ya uzalishaji wa barakoa katika Viwanda hivyo.

Bashungwa alitoa onyo kwa NGOs zilizoomba kibali cha kuzalisha barakoa kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania lakini badala yake wanauza barakoa kwa shillingi 2,500 hadi 3,000 

“wamekuwa wakitoa masharti kupitia mitandao ya kijamii kuwa hawauzi barakoa chini ya bei hiyo”.

Sitawataja kwa leo lakini nikiona tu wanauza kwa bei kubwa sitasita kuwachukulia hatua, maana mnakuja kuomba vibali kumbe mnafanya mtaji.

Aliongeza kusisitiza barakoa zote ziuzwe kwa bei isiyozidi 1500 badala ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2500 ambayo watanzania wengi inawapa changamoto ya kumudu.

Kwa upande mwingine, Bashungwa alivipongeza Viwanda nguo vya A-Z na Sunflug kwa kuzalisha barakoa ambazo zinawasaidia watanzania walio wengi, na amewahaidi serikali kuwapati ushirikiano.

Aidha alivitaka Viwanda hivyo kuendelea kuzalisha kwa wingi ili wananchi walio wengi wa vijijini waweze kupata vifaa hivyo vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa korona.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliwataka wananchi wote wa mkoa huo kuchukua taadhali zinazotolewa na Wizara ya afya wanapotembelea maeneo yenye mkusanyiko.

Pia, alisisitiza kuwa ni vema sasa wafanyabiashara hao wakatengeneza barakoa kwa bei nafuu ili kuwezesha wananchi kununua.

Wakitoa taarifa kwa Mhe. Waziri, Emmanuel Mgoma muakilishi wa kiwanda cha Sunflug alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha barakoa 25,000 kwa siku.

Muakilishi wa A-Z,  Slyvester Kazi alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha barakoa 15,000 kwa siku.


 Waziri wa Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa{kulia} akipata maelezo kutoka kwa Emmanuel Mgoma{kushoto} muakilishi wa kiwanda cha Sunflug ambacho kwa sasa kinazalisaha barakoa 25,000 kwa siku. {katikati} Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo

Waziri wa Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa akitolea ufafanuzi wa bei ya barakoa ambapo ameagiza bei isizizi 1500 badala ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2500 ambayo watanzania wengi inawapa changamoto ya kumudu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad