HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 26, 2020

WAZIRI KAIRUKI APONGEZA JUHUDI ZA BRELA

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amepongeza juhudi zinazofanywa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika kuhamasisha urasimishaji wa Biashara.

Hayo yamebainiswa leo alipohudhuria kama Mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Warsha hiyo Mhe. Kairuki amesema ni muhimu sana kwa Wajasiriamali kurasimisha Biashara kwa kuwa itafungua fursa nyingi sana.

“Kurasimisha Biashara ni muhimu sana, na ninafurahi sana kuwaona BRELA hapa, kwa sababu, urasimishaji wa biashara unakuja na fursa mbalimbali ambazo zinazaidia ukuaji na kuongeza kipato”.Alisema Mhe. Kairuki.

Naye Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa ametoa wito kwa wanawake wote wajasiriamali kusajili majina ya Biashara zao, Alama za Biashara au huduma, Usajili wa Kampuni na pia huduma zingine za BRELA.

“Natoa rai kwa wanawake wajasiriamali wote kutumia huduma za BRELA ambazo zote zinapatikana kwa njia ya mtandao. 

Huduma hizo ni pamoj na Usajili waa Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za Biashara au Huduma, Usajili wa Kampuni, Kutoa Hataza, Kutoa Leseni za Biashara Kundi A pamoja na kutoa Leseni za Viwanda”.

Aidha Bw. Chuwa ameeleza kuwa ili kuweza kufungua huduma katika mfumo wa ORS hitaji la kwanza ni kuwa na namba ya utambulisho wa Taifa kisha kutembelea www.brela.go.tz ili kupata huduma zote. 

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki akisikiliza kwa makini jambo katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
 Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya BRELA kufanikisha Tanzania ya Viwanda katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad