Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Serikali
imesema kuwa Soko la ajira rasmi nchini ni dogo sana na hivyo
halikidhi mahitaji ya wahudumu wote kwa hali hiyo wahitimu hao
wanatakiwa kukabiliana na changamoto ya Soko hilo kwa kuelekeza mawazo
yao kwenye kujiajiri badala ya kuajiriwa.
Hayo
ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina
Shaban wakati akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango katika mahafali
ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam
na Mtwara yaliyofanyika katika Viwanja vya Kampasi jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa kwa wale wahitimu wenye ajira msingi mkuu wa mafanikio ni kufanya
kazi kwa kuzingatia sera,Sheria,Taratibu na Kanunu ikiwa ni pamoja na
kujiepusha na vishawishi au vitendo vya rushwa na ubadhirifu kwa kuwa
vina madhara makubwa ya maisha ya mtu Mmoja moja na uchumi wa Taifa letu
kwa ujumla.
Shaban
amesema elimu inayotolewa na TIA imejikita kwenye fani za Uhasibu
ikiwemo Uhasibu wa Fedha za Umma, Ununuzi na Ugavi,Usimamizi wa
Biashara, Uongozi wa Rasilmali Watu pamoja na Masoko hivyo fani hiyo ni
nguzo muhimu katika kuendesha Uchumi wa Taifa hususani katika kusimamia
mapato na matumizi ya Fedha za Umma.
Naibu
Katibu Mkuu huyo amesema sera yetu kwa sasa ni uchumi wa viwanda hivyo
umahiri wa wataalam wanaozalishwa unatakiwa kuonekana ili kufanikisha
azima ya serikali ya Tanzania ya Viwanda.
Shaban
amekazia katika kukabiliana na changamoto za Usimamizi wa Mapato na
matumizi ya Fedha za Umma,mahitaji ya Soko ,Ushindani na Utandawazi
hamna budi Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) Kuendesha Shughuli kwa
kutumia Teknolojia ya Kisasa ya kupeana na kubadilishana taarifa kwani
watalaam wanaohitajika ni wenye weledi,maarifa na umahiri wa kutatua za
changamoto na si kuongeza changamoto kwa Wananchi katika kupata huduma.
Amesema
kuwa TIA izingatie umakini wa suala la umahiri katika mitaala ili
kuweza kuwa na wataalam wenye uwezo wa kulifikisha Taifa kwenye uchumi
wa Kipato cha kati kabla ya 2025.
Mwenyikiti
wa Bodi ya Wizara ya Fedha na Mipango Wakili Said Chiguma amesema kuwa
waajiri wa sekta ya Umma na binafsi wamekuwa wakiona mafanikio kwa
wahitimu wa TIA kuwa na sifa zilizotukuka katika kufanya kazi licha ya
kuwapo kwa Vyuo vingi nchini na kufanya Chuo hicho kuendelea kuongeza
idadi ya udahili kwa wanafunzi kusoma kwa kila mwaka.
Amesema Taasisi ina wanafunzi zaidi ya 19,000 katika Kampasi Sita za Kimkakati.
Nae
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Luciana
Hembe amesema kuwa wahitimu katika Chuo hicho wameweza kjfundishwa
ujasiriamali ili kuweza kujiajiri katika kukabiliana na changamoto ya
ajira nchini.
Amesema
Chuo kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakiksha wahitimu wanajiajiri
katika maeneo Mbalimbali ya kuweza kukidhi mahitaji yao pamoja Taifa
kunufaika na maarifa yao ya kujiajiri.
Aidha
amesema kuwa Baadhi wahitimu katika Taasisi hiyo wa miaka iliyopita
wameweza kuanzisha Kampuni mbalimbali ambazo ziko katika Ushindani wa
kibiashara na Kampuni zingine.
Amesema
wahitimu wa mwaka 2019 nao watumie ujuzi na maarifa yao katika kufungua
milango ya ajira ya kujiajiri ili wasitumie muda mwingi wa kusubiri
ajira katika sekta ya Umma na binafsi.
Mwenyikiti
wa Bodi ya Ushauri wa Wizara ya Fedha na Mipango Wakili Said Chiguma
akitoa maelezo kuhusiana na uendeshaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania
(TIA) katika Mahafali ya 17 yaliyofanyika katika Viwanja vya Taasisi
hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban akizungumza
katika Mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika
katika Kampasi Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja na baadhi Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
Baadhi
ya Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakifatilia Hutuba ya
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Viwanja
vya Kampasi Kuu ya Jijini Dar es Salaam.
baadhi
ya Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiwa katika mahafali
ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Viwanja vya Taasisi jijini Dar es
Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya Ushauri wa Wizara ya Fedha na Mipango Thabit Dokodoko akitoa
shukurani kwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) yaliyofanyika Viwanja Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban
akiwa katika picha ya pamoja na Meza Kuu mara baada ya kuhitimisha
mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliofanyika katika
Kampasi Kuu ya Dar es Salaam.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Luciana Hembe
akitoa akizungumza na waandishi habari mara baada ya kuhitimishawa kwa
Mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment