HUDUMA YA MAJI KIGAMBONI YAENDELEA KUBORESHWA- DAWASA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 14, 2019

HUDUMA YA MAJI KIGAMBONI YAENDELEA KUBORESHWA- DAWASA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Katika  kuboresha huduma ya maji safi kwa wakazi wa Kigamboni Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira DAWASA wametembelea miradi ya maji ya Kijamii inayosimamiwa na Mamlaka hiyo.

Katika ziara hiyo waliongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambapo akiweza kutembelea miradi mbalimbali inayotoa huduma na ile iliyo katika hatua za mwisho za umaliziaji.

Luhemeja ametembelea miradi ya visima iliyopo Kigamboni ikiwemo moja ya Kisima kutoka kwenye Mradi wa Kimbiji na Mpera  kinachojengwa na Kampuni ya Serengeti.

Baada ya kutembelea kisima hicho cha K13, Luhemeja ameweza kushuhudia majaribio ya kuvuta maji (pump testing) ambacho kimekamilika tayari kwa kuanza mchakato wa ulazaji wa mabomba ya kusafirishia maji na yale ga usambazaji.

Ziara hiyo imefanyika leo ikiwa ni katika kuhakikisha mji wa Kihuduma Kigamboni unapata huduma ya maji safi kutoka Mamlaka hiyo

Mbali na kisima hicho, Luhemeja ametembelea pia mradi wa maji wa Kisima Minondo kikiwa na tanki la ujazo wa Lita 45,000, Mradi wa Kisima cha Gezaulole chenye matanki mawili ya ujazo wa Lita  45,000 na Lita 90,000.

Luhemeja, pia ametembelea mradi wa Kisima cha Kibugumo chenye uwezo wa kuzalisha lita za maji 6800 kwa saa.

Pia, ameweza kutembelea nyumba za NSSF zilizopo Kijichi  Vikunai ambazo Dawasa wanatarajia kupelekea maji kwenye nyumba hizo ili wakazj wa eneo hilo wafaidike kwa kupata huduma ya maji kutoka Dawasa.
Mmoja wa wafanyakazi kutoka kampuni ya Serengeti inayochimba mradi wa maji wa Visima vya Kimbiji na Mpera akifungua koki ili kuruhusu maji wakati wa Pump testing leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akijaribu maji kutoka katika ch K13 kiyakachihudumia mkoa wa kihuduma Kigamboni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuini ya Serengeti Mehrdad Talebi baada ya kutembelea mradi wa Visima vya Kimbii na Mpera na kushuhudia majaribio ya kuvuta maji (pump testing) ambacho kimekamilika tayari kwa kuanza mchakato wa ulazaji wa mabomba ya kusafirishia maji na yale ga usambazaji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuini ya Serengeti Mehrdad Talebi baada ya kutembelea mradi wa Visima vya Kimbii na Mpera.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya baada ya kutembelea moja ya miradi ya kijamii inayofanyiwa ukarabati na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Kigamboni, wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya kijamii katika mkoa wa kihuduma Kigamboni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya baada ya kutembelea moja ya miradi ya kijamii  inayotoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa kihuduma Kigamboni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Dawasa Neli Msuya baada ya kutembelea moja ya miradi ya kijamii  inayotoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa kihuduma Kigamboni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo kwa watendaji wa Mamlaka hiyo ya kuhakikisha wanafikisha maji katika nyumba za NSSF ziizopo katika hatua ya umaliziaji ili wakazi wa eneo hilo wanufaike kwa kupata huduma ya maji safi kutoka Dawasa.
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma Kigamboni wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Tumaini Muhondwa  akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa   Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya kijamii katika mkoa wa kihuduma Kigamboni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad