HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 4, 2019

WATOA HUDUMA ZA MAJI WAKABIDHIWA VYETI, WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA MPYA YA 2019

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamewataka watoa huduma za majisafi kuzingatia sheria mpya ya maji na usafi wa mazingira namba 5 ya mwaka 2019.

Hayo yamesemwa leo wakati wa hafla fupi ya utoaji vyeti kwa watoa huduma za maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.

Lengo la hafla hiyo ni pamoja na kuwatambua na kuwapa vyetu vya uendeshaji iliyoandaliwa na DAWASA.

Akizungumza kabla ya kukabidhiwa vyeti hivyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe amesema sheria mpya ya maji inawataka kutoa huduma yenye ubora unaofanana na inayotolewa na DAWASA.

Amesema, baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo watoa huduma za maji watakuwa na uhuru wa kusambaza majisafi katika maeneo yao na wanatambulika na DAWASA kwenye maeneo yao.

"Watoa huduma watatakiwa kutunza miundo mbinu katika hali ya ubora na usafi, kupima ubora wa maji na kutunza orodha ya wateja.,"amesema Mkwanywe na kuongeza kuwa masharti hayo siyo magumu kwa mtoa huduma yoyote makini´

"Naamini hakuna atakayeshindwa kuyatekeleza hasa ukizingatia kwa sasa hapatakuwa na kodi wala tozo lolote kutoka DAWASA, usumbufu wala changamoto ya kuongeza muda wa cheti endapo masharti yote yakifuatwa"

"Nafurahi kusikia kuwa mmepima na kujihakikishia ubora wa maji pamoja na miundo mbinu yenu imekaguliwa na taarifa muhimu za kiundeshaji zimepatikana, hivyo sasa mpo tayari kuwa wawakilishi wetu wazuri maeneo mnayoyahudumia,"amesema.

Mkwanywe amewaasa watoa huduma kufuata sheria hususani baada ya kupata vyeti na kuwa upo mkono wa sheria kwa wale wachache ambao watakwenda kinyume na taratibu za nchi za usimamizi wa huduma ya majisafi na wale watakaokiuka hawataongezewa muda wa cheti baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Neli Msuya akitoa mafunzo kabla ya utoaji wa vyeti alisema, kutakuwa na utaratibu wa kuratibu huduma za maji safi, ubora wa maji, usawa na upatikanaji, udhibiti wa usafi wa mazingira.

DAWASA wamekuwa wanafanya semina ili kutoa elimu na ufahamu wa jinsi DAWASA wanavyofanya kazi na pia kuelelezana njia bora za kuboresha ubora wa huduma za DAWASA.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe akizungumza na watoa huduma za Majisafi kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar ikiwa ni hafla maalumu ya kuwatambua na kuwapa vyeti vya uendeshaji.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii, Neli Msuya akizungumza na watoa huduma za Majisafi kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar ikiwa ni hafla maalumu ya kuwatambua na kuwapa vyeti vya uendeshaji.
Mtaalamu wa maabara Maliweza Shusha akizungumzia ubora wa maji kwa watoa huduma za maji na umuhimu wa kupima na kujihakikishia ubora wa maji ikiwemo kusafisha visima na matanki pale inapohitajika. Hayo aliyasema wakati wa hafla fupi ya utoaji vyeti kwa watoa huduma za maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe akikabidhi vyeti kwa watoa huduma za Majisafi kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar ikiwa ni lengo la kuwatambua na kuwapa vyeti vya uendeshaji. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii, Neli Msuya.

Watoa huduma za maji wakiendelea kupata elimu ya maji na kufahamu sheria mpya ya mwaka 2019 kabla ya hafla fupi ya utoaji vyeti kwa watoa huduma za maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.
Picha zote na Zainab Nyamka.




















































































No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad