WASANII WATEMBELEA MIRADI YA DAWASA, WAUPONGEZA UONGOZI WA AWAMU YA TANO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 12 October 2019

WASANII WATEMBELEA MIRADI YA DAWASA, WAUPONGEZA UONGOZI WA AWAMU YA TANO

Na  Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii

Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania wameupongeza uongozi wa awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa za kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Wasanii hao wamefanya ziara ya kutembelea miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) iliyopo Jijini na kwenye mtambo wa Ruvu juu na Mtambo wa Ruvu Chini.

Katika ziara hiyo, wasanii hao wamepata elimu na kujionea hatua za uzalishaji maji kuanzia mwanzo hadi maji yanapokwenda kwa mtumiaji.

Waliweza kupata elimu ya uzalishaji maji kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Aron Joseph ambapo amewaonesha hatua zote kuanzia yanapochukuliwa kwenye Mto Ruvu hadi hatua ya mwisho na tayari kwa matumizi.

Akizungumzia ziara hiyo iliyoandaliwa na DAWASA, Katibu wa Chama hicho Halima Yahya 'Davina' amesema wamefurahi kuona maendeleo makubwa sana katika sekta ya maji na juhudi kubwa zimefanywa na serikali ya awamu ya tano.

Davina amesema,wameshuhudia mitambo mikubwa, ambapo wameweza kupata elimu juu ya uzalishaji maji na kiasi kinachozaliwa kutoka kwenye vyanzo hivyo vya maji.

"Tunaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa wanayoifanya, tumeona mambo makubwa yaliyofanywa na katika yote tumeona hapa Mtambo wa Ruvu Chini jumla ya Lita Milion 270 zinazalishwa kwa siku ambapo ni jambo kunwa sana," amesema Davina.

"Kulikua na shida ya maji na kazi kubwa iliyofanywa ni kuhakikisha wananchi wote wanapata majisafi na salama, kwani wakina mama sisi ndio wahanga wakubwa wa maji pindi yanapokosekana ila juhudi za Rais tunaona mafanikio yake na kwa upande nachagua mafanikio," amesema.

Mmoja wa wasanii hao Snura Mushi amesema kama kuna uwezekamno wa kuongeza asilimia na kuupongeza  uongozi wa serikali ya awamu ya tano ni jambo la Kumtua mama ndoo kichwani.

Snura amesema, Dawasa wamefanikiwa katika masuala mengi na wamefanikisha kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi hasa mkoa wa Dar es Salaam.

Wasanii hao kwa pamoja wamewaomba wananchi kulipa ankara za bili ya maji kila mwezi ili kufanikisha Mamlaka hiyo kuendelea kujenga miundo mbinu mipya ya maji na kufikia asilimia 95 ya wakazi wa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Pwani ifikapo mwaka 2020.

Maeneo waliyotembelea wasanii hao wa filamu ni Tenki la Maji la Chuo Kikuu lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni 43, tenki la maji Changanyikeni la ujazo wa Lita Milioni 5 na kituo cha Kusukumia maji, tenki la Salasala, Mtambo wa Ruvu Chini na Mtambo wa Ruvu Juu.


Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania wakipata maelekezo kutoka wa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya baada ya kutembelea tenki la maji la Chuo Kikuu ikiwa ni ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na DAWASA 
 
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Aron Joseph akitoa maelezo kwa Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania baada ya kutembelea tenki la Changanyikeni na kituo cha kusukumia maji cha Makongo ikiwa ni ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na DAWASA .
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Aron Joseph akielezea jinsi mashine zinavyofanya kazi baada ya kupokea kutoka Mtoni, maelezo hayo ameyatoa kwa Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania waliotembelea Mtambo wa Ruvu chini. 
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Aron Joseph akitoa maelezo kwa Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania baada ya kutembelea mtambo wa Ruvu Chini  ikiwa ni ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na DAWASA 
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Aron Joseph akitoa maelezo kwa Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania baada ya kutembelea mtambo wa Ruvu Chini  ikiwa ni ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na DAWASA 
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Mhandisi Aron Joseph akitoa maelezo kwa Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania baada ya kutembelea mtambo wa Ruvu Juu ikiwa ni ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na DAWASA
Picha ya Pamoja ya Uongozi wa DAWASA na Chama cha Wanawake watasnia ya Filamu Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad