HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 8, 2019

DC KINONDONI AFANYA ZIARA MBEZI JUU KUKAGUA UTEKELEZAJI WA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI

Na Ripota Wetu,Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo amefanya ziara katika Kata ya  Mbezi Juu kwa lengo la kujionea utekelezaji wa utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa eneo hilo.

Akizungumza akiwa katika Kata hiyo leo Oktoba 8, 2019  Chongolo amesema amefanikiwa kuona kinachoendelea kwa sasa katika kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa Mbezi Mtoni na maeneo yanayozunguka eneo hilo.

" Tumekubaliana na DAWASA Kawe kushughulikia changamoto hizo kwa haraka, nami baada ya wiki mbili nitarudi tena kuangalia maendeleo ya kazi ya kuwafikishia maji wananchi. Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Jemedari wetu Rais John Magufuli ni kuhakikisha kuwa wanaKinondoni wote wanapata maji safi na salama ifikapo 2020,"amesema

Ameongeza kuwa mpaka sasa tupo zaidi ya asilimia 80 na kuongeza matanki matano yamekamilika na kila moja lina uwezo wa kihifadhi lita milioni sita." Mungu ni mwema, kwani ni hakika mama wa Kinondoni ikifika 2020 atasahau kubeba ndoo ya maji kichwani,".
 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akielezwa jambo kutoka kwa mmoja wa Wafanyakazi wa DAWASA Kawe, akiwa kwenye ziara yake katika Kata ya  Mbezi Juu kwa lengo la kujionea utekelezaji wa utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa eneo hilo.
 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akimsikiliza mmoja wa Wananchi wanaoishi katika eneo hilo la Mbezi Juu kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad