HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 18, 2019

Wageni wa SADC wavutiwa na huduma bora za TMA

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutokana na ubora wa huduma zao, umevutia wageni  kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Akizungummzia ubora wa huduma zao leo Septemba 18,2019, Kaimu Meneja wa Huduma za Utabiri TMA, Wilberforce Kikwasi amesema kutokana na taarifa zao kuwa na ukweli wa zaidi ya asilimia 80, kumekuwa na kasi kutoka kwa wataalam wa hali ya hewa kutoka SADC wanaotembelea banda la mamlaka hiyo.

Amesema  katika mkutano huo watawaonyesha wataalamu wenzao  namna wanavyofanya kutafuta, kuchakata na kutoa taarifa za hali ya hewa kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Kikwasi, TMA pia imepata uzoefu kwenye mkutano huo kwa nchi zinazopata majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Nchi yetu inatumika kimkakati katika ukanda huu na hii ni kutokana na miundombinu tuliyonayo ambayo serikali imetusaidia sana. Wananchi hapa nchini wana nafasi kubwa ya fursa za kiuchumi kwa kufuatilia na kuzitumia taarifa za hali ya hewa," amesema Kikwasi.

Ameongeza kuwa biashara  zinategemea sana taarifa za hali ya hewa na shughuri nyingine pia za kimaendeleo hivyo, TMA inawashauri wananchi wafuatilie taarifa wanazozitoa.

Amesema maendeleo ya wakati ujao kwa Tanzania, SADC na nchi zote za Afrika zinategemea zaidi taarifa za hali ya hewa hivyo wadau na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuzifuatilia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad