SUMATRA PWANI YABANA MAGARI YANAYOKATISHA RUTI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 30 September 2019

SUMATRA PWANI YABANA MAGARI YANAYOKATISHA RUTI

 NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MAGARI ya abiria kumi,yafanyayo safari zake Mbezi -Tumbi na Mbezi-Mlandizi yamekamatwa na kupigwa faini ya sh.100,000 kutokana na kukiuka kosa la kukatisha ruti.

Aidha magari yafanyayo safari zake Bagamoyo -Tegeta Nyuki na Kisarawe yametakiwa kutoza nauli zilizowekwa kisheria ili kuondoa malalamiko kwa abiria.

Akielezea kuhusu taarifa hiyo, ofisa mfawidhi SUMATRA,Mkoa wa Pwani ,Omary Ayubu alisema, wanatekeleza maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Pwani baada kupokea malalamiko na kuomba watatue tatizo la kukatisha ruti.

Alieleza , magari matatu yamekatisha ruti kutoka Mbezi - Tumbi ambayo yaligeuzia Njuweni na mengine saba yaligeuzia Kongowe.

Ayubu alisema ,wataendelea kuwachukulia hatua kali madereva na wamiliki wa magari hayo ili iwe fundisho kwa wengine ambapo mbali ya faini watapaswa kuzingatia taratibu za leseni zao pasipo kugeuza njiani.

" Zoezi hili ni endelevu ,hatuishii hapa ,licha ya mkuu wa mkoa kutoa maelekezo lakini na sisi tumejipanga kushirikiana na jeshi la polisu kupitia kikosi cha usalama barabarani."

"Wamiliki wajieleze kwa siku saba ,kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua kali ya kufungiwa leseni au kufikishwa mahakamani."Alibainisha Ayubu.

Akieleza kuhusu magari ya abiria yanayokwenda Bagamoyo kupitia Baobao alisema, wanaendelea kusisitiza wamiliki kuona umuhimu wa barabara hiyo.

Ayubu alifafanua, nayo magari yanayofanya safari zake Makumbusho-Tegeta Nyuki na njia ya kwenda Kisarawe waache kuzidisha nauli wafuate sheria na nauli zilizopangwa bila kuwaumiza abiria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad