HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 17, 2019

SERIKALI YAJA NA MCHAKATO MADHUBUTI WA UPIMAJI VIRUSI VYA UKIMWI BINAFSI

Na Jusline Marci-Arusha.

Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe.Dkt. Faustine Ndungulile amesema serikali ipo katika mchakato wa kuleta mpango madhubuti wa upimaji virusi vya UKIMWI binafsi.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha tathimini juu ya namna ya kupunguza maambukizi ya UKIMWI Tanzania kilichoandaliwa na Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Jijini Arusha.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa mfumo wa upimaji binafsi unalenga kuwafikia zaidi makundi ambayo yapo kwenye mazingira hatarishi hasa ya vijana wakike na pia kutoa wigo mpana kwa wanaume na kuwapima kwani bado idadi yao ni ndogo ukilinganisha na wanawake.

Aidha amesema serikali katika kuhakikisha inatokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2016 imeweka mkakati uitwao 90, 90,90 yani (asilimia 90 ya watu wanatakiwa wawe wanajitambua hali zao,asilimia 90 waanze kutumia dawa na asilimia 90 kuhakikisha wamefubaza VVU).

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Arusha mkakati huu umeweza kufanya vizuri sana kwa asilimia 90 ya kwanza kufanikiwa kwa asilimia 76,asilimia 90 ya pili kufanikiwa kwa asilimia 98 na asilimia 90 ya tatu imefanikiwa kwa asilimia 80.

Pamoja na hayo amesema serikali itaendelea kuboresha baadhi ya huduma kama vile; kuongeza muda wa uchukuaji dawa za kupungaza makali ya UKIMWI kutoka miezi 3 hadi 6 pamoja na kutoka mafunzo kwa baadhi ya wataalamu wa afya ili kuongeza wigo wa utoaji huduma.

Sambamba na hilo katika kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa na serikali ifikapo 2030 na ugonjwa huo umetokomezwa kabisa na serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi zote za serikali na binafsi zilizojikita katika kutokomeza ugonjwa huo.

Nae makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya huduma ya maendeleo ya jamii Mhe. Juma Nkamia ambapo amezishauri taasisi zote zinazoshughulika na tafiti za mapambano dhidi ya UKIMWI na kuhakikisha zinatumia lugha ya Kiswahili kama lugha kuu ya mawasiliano ili jumbe ziweze kuwafikia walengwa kwa urahisi zaidi na kueleweka.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya bianadamu Profesa Yunus Mgaya, amesema lengo la tafiti mbalimbali zinazofanywa na NIMR ni kuhakikisha zinasaidia malengo mbalimbali ya wizara ya afya na kurekebisha sera kwa manufaa ya nchi kwa ujumla.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR), Jijini Arusha waliohudhuria mkutano huo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad