RAIS DKT. MAGUFULI AMPA POLE MKUU WA MAJESHI JENERALI VENANCE MABEYO AMBAYE AMEFIWA NA MTOTO WAKE NELSON MABEYO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 23 September 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AMPA POLE MKUU WA MAJESHI JENERALI VENANCE MABEYO AMBAYE AMEFIWA NA MTOTO WAKE NELSON MABEYO


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Ndugu Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwake Msasani mara baada ya kufiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mama Mabeyo ambaye amefiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza sala pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na familia yake wakimuombea marehemu   Nelson Mabeyo ambaye alifariki kwa ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad