HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 19, 2019

DAWASA YATOA ONYO KWA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) leo Septemba 19 imekagua miundombinu ya maji katika Mikoa ya kihuduma ya Mtaa wa Dovya, Bunju na kushuhudia wananchi wakihujumu maji kwa kutengeneza mabwawa ya umwagiliaji na kusababisha hasara kwa wateja halali waliounganishwa na wanaolipa bili.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu ya maji katika kata ya Bunju mtaa wa Dovya jijini humo meneja mapato wa DAWASA Edger Zawayo amesema kuwa bado wanaendelea  miundombinu ya DAWASA na wamethibitisha mabwawa wanayotumia kustawisha mazao yao ni ya DAWASA na wamiliki wa mabwawa hayo wamekimbia.

Amesema kuwa kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake kwa kutoa taarifa kwenye ofisi za Serikali za mitaa na ofisi za DAWASA zilizokaribu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

"Ukikutwa unahujumu miundombinu ya maji faini ni kuanzia shilingi milioni tano hadi hamsini, hivyo ni vyema wananchi wakatumia fedha hizo kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kupata huduma hiyo ya maji kwa halali kabisa" Ameeleza Zawayo.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa mtaa wa Dovya Clara Kiriho amewaasa wananchi wa Dovya juu wa wizi wa maji wanaoufanya na kutumia maji hayo kumwagilia bustani badala yake wafuate taratibu maalumu na kupata huduma hiyo ya maji kwa uhalali.

Amesema kuwa wananchi wote wanaohitaji huduma ya maji ofisi zipo kila mahali ni vyema wakafuata taratibu na kulipa bili na sio kuhujumu maji kwa wateja halali na kuwasababishia hasara. 


 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo(kulia) akimsikiliza Mtendaji wa mtaa wa Dovya Clara Kiriho alipokuwa anatolea ufafanuzi wa matumizi ya kiwanja hicho kinacholimwa Mbogamboga na wananchi wanaoiba maji ya Mamlaka hiyo katika mtaa wa Dovya kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo.
 Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam (DAWASA) Mohammed Mwakimila akionesha mambomba ya maji yaliyokuwa yanaunganishwa kwenye bomba la Mamlaka hiyo na kuelekezwa kwenye kisima na kumwagilia mbogamboga wakati wa ziara ya kushtukiza kwenye shamba lililopo kata mtaa wa Dovya kata ya Bunju jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji wa mtaa wa Dovya Clara Kiriho (katikati) akitolea ufafanuzi kwa Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo(kulia) walipokuwa waangalia mbogamboga zilivyostawi kwenyeshamba hilo lililokuwa linatumia maji ya wizi ya DAWASA.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akikagua mambomba yanayotumiwa na na wananchi hao kama niya DAWASA au la mara baada ya kufanya ukaguzi wa kustukiza kwenye shamba hilo na kukuta wizi wa maji kwa kiasi kikubwa katika mtaa wa  Dovya kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya visima vya maji vinavyotumika kuhifadhia maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam (DAWASA) vilivyokutwa katika shamba la mbogamboga katika mtaa wa  Dovya kata ya Bunju jijini Dar es  Salaam leo.
Shamba la Mbogamboga likiwa limenawili kwa kutumia maji ya wizi ya DAWASA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad