DAWASA YAENDELEA NA MSAKO WA WEZI WA MAJI MKOA WA KIHUDUMA KAWE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 28 September 2019

DAWASA YAENDELEA NA MSAKO WA WEZI WA MAJI MKOA WA KIHUDUMA KAWE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam imewataka wananchi kujisalimisha kwenye ofisi za mamlaka hiyo ili waweze kuunganishiwa maji kiuhalali na kuacha kuchepusha  kwani ni kosa kisheria.

DAWASA wameendelea na ukaguzi wa miundo mbinu ya maji inayohujumiwa na wananchi wasio waaminifu na kusababisha mamlaka kupata hasara.

Zoezi hilo limekuwa endelevu kwa Mkoa wa kihuduma DAWASA Kawe na kufanikiwa kugundua maeneo ya watu mbalimbali wakiwa wanaunganisha maji kwa njia wa wizi.

Matukio ya wizi wa maji yameendelea kuvumbuliwa kwa kasi kubwa ambapo jitihada za Mamlaka zimefanikiwa kuwakata watu mbalimbali wanaohujumu miundo mbinu na kulipa hasara Mamlaka.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanikiwa kugundua wizi wa maji katika eneo la Maringo Kawe, Fundi Mita Idara ya Biashara DAWASA Martin Kilembe amesema wameweza kupata taarifa ya wizi wa maji katika maeneo haya na wamechunguza na kugundua wizi mkubwa unaofanywa kwa kujiunganishia maji nyuma ya mita ya maji.

“kujiunganishia maji nyuma ya mikta ni kosa kisheria unakuwa unahujumu shirika na utakapobainika sheria itachukua mkondo wake, eneo hili lote lilikuwa ni la mtu mmoja na lina mita nne za maji ambapo mita mbili tulishawakatia maji na mita mbili zingine zinaendelea kufanya kazi,”amesema Kilembe.

“Katika mita zilizobaki kuna moja inahudumia sehemu ya kuoshea magari (Car wash), nyingine inahudumia nyumba hii na zingine zilishakatiwa maji ila tumeona wanaendelea kupata maji”

Kilembe amesema, wamegundua sehemu walikofanya maunganisho ya maji na wamekuwa wanafanyia ujenzi wa ukumbi wa starehe lakini mita yao ikiwa imekatwa na inaonesha maunganisho ya maji wanayotumia kutoka katika bomba kuu lililopo nyuma ya jengo hilo.

"Ni kosa kisheria, na mteja anaunganisha maji nyuma ya mita anakuwa amefanya hujuma na hasara kwa serikali na makosa haya yanapelekea kulipa faini au kufunguliwa kesi na kupelekwa mahakamani na atalipa gharama zote za uharibifu uliofanywa," 

Kilembe amesema, miundo mbinu hii ni ya muda mrefu na kipindi cha nyuma mita za maji zilikuwa zinafungwa kwa ndani, sasa kuna haja ya kuanza kupitia maeneo yote na mita hizo zitolewe nje.

DAWASA imeendelea kuwataka wananchi kuacha kuhujumu miundo mbinu ya maji kwani utakapokamatwa sheria itachukua mkondo wake na hakutakuwa na huruma kwa mtu yoyote na faini ni kuanzia miaka 5,000,000 hadi milioni 50 au kifungo kisichopungua miaka saba au vyote viwili.

Wateja wa DAWASA wameombwa kuacha kuchepusha maji na zaidi wajisalimishe kwenye mamlaka ili kuweza kupata huduma ya maji kwa uhalali na kuacha kuhujumu miundi mbinu ya Mamlaka.
Mita ya maji jnayohudumie eneo la Car Wash ikiwa ndani ya uzio wa nyumba iliyokutwa imechepusha maji.
Fundi Mita Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akisoma mita ya maji iloyopo ndani ya uzio mmoja ambapo kwa mujibu wa wasoma mita haina tatizo lolote na imekuwa inalioiwa kila mwezi, zoezi hilo limefanyika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe.
Fundi Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akionesha mita ya maji iliyokatwa ila ujenzi wa maji ukiwa unaendelea kwa kutumia maji ya DAWASA.
Jengo linalojengwa kwa kutumia maji ya wizi kitoka DAWASA.
Fundi Mita kutoka Idara ya kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akitoa maelekezo kwa mafundj wa DAWASA wakati wa zoezi la kutafuta maunganisho ya maji yanayopeleka maji kwa mmiliki wa jengo la burudani anayotumia kwa ajili ya ujenzi, zoezi hilo limefanyika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe.
Fundi wa DAWASA akionesha maunganisho ya maji nyuma ya mita yanayopeleka maji kwenye jengo linalojengwa la ukumbi wa burudani wakitumia kwa ujenzi.
Fundi Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuendelea kuwatafuta wanaohujumu miundo mbinu ya maji kwa kuchepusha maji na kulipa hasara mamlaka na serikali kwa ujumla zoezi hilo limefanyika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe.
Picha Zote na Zainab Nyamka


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad