DAWASA YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI MTAA WA KILUNGULE KATA YA BUNJU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 17 September 2019

DAWASA YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI MTAA WA KILUNGULE KATA YA BUNJU

UHUJUMU wa Miundo mbinu unasababisha upotevu wa pesa na kusababisha maeneo mengine isiyokuwa na mtandao wa maji kukosa huduma kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa waaminifu.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameendesha ukaguzi wa miundo mbinu katika Mikoa ya  kihuduma Dawasa wakianzia Kawe katika Mtaa wa Kilungule Bunju na kukuta wananchi wakihujumu miundo mbinu ya maji.

Hayo yamesemwa na Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo baada ya kutembelea Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe na kukuta wananchi wakijiunganishia maji kwa wizi.
Amesema, wananchi wamekuwa wanakosesha Mamlaka mapato na kusababisha miundo mbinu mingine kushindwa kujengwa, kusogeza maji kwa wananchi pamoja na kuboresha miundo mbinu mingine.

Zawayo ameeleza kuwa, katika eneo waliloanza kutembelea wamekuta wananchi wamejiunganishia maji kukiwa na mita mbili,  ambapo inayosoma ni moja na nyingine ikiwa haisomi huku wakijaza mabwawa ya maji na kupelekea maji kupotea na kulipa hasara Mamlaka.

“huu ukaguzi ni ili tuweze kuwabaini wale wote wanaohujumu miundo mbinu ya maji ambapo wanasababisha Mamlaka kushindwa kuendeleza miradi mingine, tumekuta wananchi hapa wanatumia maji yanayolipiwa ni kidogo tofauti na yale yasiyolipiwa ambapo wamekuwa wanamwagilia mboha mboga,” amesema Kulumbe

Aidha, amewaomba wananchi kuacha kuhujumu Mamlaka zaidi maji yote wanayotumia yapite kwenye mita zinazotambulika ili Mamlaka isipate  hasara na zaidi wale wote watakaokamatwa kwa makosa ya kujiunganishia maji kiholela watachukuliwa hatua za kisheria na kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake.

Kwa upande wa  Mtendaji wa Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju, Abdalla Mbupu amesema wananchi waache kutumia maji bila kufuata utaratibu na kusababisha serikali kukosa mapato ili DAWASA waweze kuendelea na uwekezaji wa miundo mbinu ya maji.

“Jambo wanalolifanya DAWASA ni zuri sana, na kinachoonekana ni tatizo na kumekuwa na upotevu wa pesa na wito kwa wananchi ni kuacha hizo tabia wafuate utaratibu na kuacha kutumia maji bila kulipia ikiwemo kumwagilizia maji mbogamboga,”

Mbupu amewasishi wananchi kuacha mara moja kuihujumu na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali ya mtaa au ofisi za DAWASA pindi wanapoona mmoja anatenda kosa la kujiunganishia maji.

Zoezi hilo litakuwa endelevu katika Mikoa 10 ya kihuduma DAWASA ambapo wataendelea na ukaguzi wa maeneo mbalimbali ili kubaini wale wote waliojiunganisia maji kiholela na kusababisha mamlaka hiyo kupata hasara.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo  akionesha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo pamoja na waandishi wa bomba hilo lililounganishwa kinyemela linapoelekea mara baada ya kugundua na kukatwa kwa Bomba la DAWASA.
 Muonekano wa Bomba la DAWASA likiwa limekatwa baada ya kugundulika kwa wizi wa maji ya kujiunganishia kiholela wakati wa Maafisa wa Mamlaka hiyo kufanya ukaguzi wa Miundombinu katika Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam DAWASA Martin Kulembe(kulia) akionesha Mafundi wa Mamlaka hiyo na waandishi wa habari  moja ya mota iliyokuwa inatumika kuvuta maji ya wizi kutoka kwenye bomba la  DAWASA eneo la  Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo
 Mfanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) akiangalia Bomba pamoja na Maji kama ni ya Mamlaka hiyo mara baada ya kukuta kisima hicho wakati wa kufanya ukaguzi wa Miundombinu ya Mamlaka hiyo eneo la Mtaa wa Kilungule Kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo  akionesha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo pamoja na waandishi(hawapo pichani) moja ya tenki la Maji lililokuwa linatumika kutunzia maji ya Wizi kwa ajili ya umwagiliaji wa Mbogamboga katika Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Mabwawa yaliyokuwa yanatumika kutunzia maji yaliyokuwa yanaibiwa kutoka kwenye bomba la maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
 Bomba la maji lililounganishwa kinyemela  kutoka kwenye bomba la maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) likitoa maji kwenye moja ya Shamba la mbogamboga.

 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakikata maji kwa mmoja wa wezi wa maji mara baada ya kukuta maungio yasiyoeleweka karibu na Mita ya maji ya Mamlaka hiyo leo katika eneo la Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Mashamba yaliyokuwa yaliyaliyokuwa yanamwagiliwa na Maji ya wizi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufanya ukaguzi wa miundo mbinu ya Mamlaka hiyo katika Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju jijini Dar es Salaam.
Mtendaji wa Mtaa wa Kilungule kata ya Bunju, Abdalla Mbupu akizungumza na wandishi wa habari kwa kuwasisitiza wananchi kuacha mara moja kuihujumu na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi za serikali ya mtaa au ofisi za DAWASA pindi wanapoona mmoja anatenda kosa la kujiunganishia maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad