Asasi za Kiraia waaswa kufanya kazi kwa uwazi na Uzalendo nchini - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 11 September 2019

Asasi za Kiraia waaswa kufanya kazi kwa uwazi na Uzalendo nchini

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Asasi za kiraia nchini zimetakiwa kuwa na Uzalendo,uwazi pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali kwani kufanya hivyo watasaidia kuleta mchango wa kuinua maendeleo na kukuza uchumi hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kuratibu na sekta na Asasi kutoka TAMISEM Dkt.Andrew Komba I Wakati wa Ufunguzi wa wiki ya Asasi za Kiraia inayotarajia kuanza rasmi Novemba 4 hadi 8 mwaka huu jijini Dodoma.

Amesema kuwa asasi za kiraia hapa nchini zinatoa mchango mkubwa kwa serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kuwafikia na kutoa huduma kwa wananchi jambo linalosaidia wananchi kupata maendeleo wao binafsi na taifa kiujumla.

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Asasi za kiraia Francis kiwanga  ameeleza ushirikiano kati ya asasi za kiraia,Serikali pamoja na wadau wengine wa kimaendeleo ni muhimu kwani ni moja ya njia ambayo itazisaidia asasi hizo kukua zaidia maendeleo wa binafsi pamoja na serikali kiujumla hivyo wataendelea kushirikiana na serikali katika kila sekta ili kuzitatua kero na matatizo mbalimbali ya wananchi.

Aidha ameongeza kuwa wiki ya asasi za kiraia itaanza rasmi Novemba 4 mpaka 8 mwaka huu jijini Dodoma na kauli mbiu ya wiki hiyo ni  kwa maendeleo ushirikiano ni nguzo muhimu ya maendeleo kwa Tanzania.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta wa Ofisi ya Rais-Tamisemi Dkt. Andrew Komba akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sherika la Foundation (FCS) Francis Kiwanga akizungumza kuhusiana na wiki ya Asasi Kiraia walivyipanga katika wiki itakapoanza Mjini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanganyika Law Sociaty (TLS) Kaleb Gamanya akitoa maelezo walijipanga katika utoaji wa elimu katika eneo la sheria katika wiki ya Asasi za Kiraia itakayofanyika Mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Asasi za Kiraia.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta wa Ofisi ya Rais-Tamisemi Andrew Komba akikata utembe kuashiria kufuanga wiki ya Asasi za Kiraia katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na viongozi wa Asasi za Kiraia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad