HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 6, 2019

WANANCHI WAPATA CHETI CHA KUZALIWA NANENANE SIMIYU

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Umeandaa zoezi la kusajili na kutoa cheti cha kuzaliwa kwa kila mwananchi asiyekuwa nacho                                         

Zoezi hilo lililoanza hivi karibuni linafanyika katika viwanja vya nanenane, Nyakabindi mkoani Simiyu.

Akiongea kutoka katika banda la RITA, Afisa Usajili Mwandamizi kutoka RITA Bw. Richard Ndeka anasema kuwa "RITA imejipanga vizuri kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wale wote ambao wamezaliwa Tanzania Bara lakini hawana cheti cha kuzaliwa hivyo tunawasihi wananchi hao  wajitokeze kwa wingi katika banda letu la RITA lililopo hapa viwanja vya Nyakabindi,Simiyu". 

Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu inayotumika katika nyanja mbalimbali za mahitaji ya binadamu kama vile elimu, ajira,kupata mikopo ya elimu ya juu, bima ya afya, pasi ya kusafiria n.k. Hatahivyo cheti hiki kinaonesha utambulisho wa kwanza wa mwananchi mwenyewe kwa maana ya mahali alipozaliwa, majina ya mtoto, majina ya wazazi,tarehe ya kuzaliwa pamoja na ubini wa muhusika. 

Nae Afisa Habari wa RITA, Bi. Grace Kyasi amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa huduma nyingi zinazohitaji mtu awe na cheti cha kuzaliwa imepelekea asilimia kubwa ya wananchi kuona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na cheti hicho mapema. "Cheti cha kuzaliwa kimekuwa kikitumika kupata huduma mbalimbali kama vile kupata elimu ya msingi,sekondari, kupata huduma ya afya,kupata ajira katika taasisi za Serikali, jeshini na sekta binafsi. Hata hivyo cheti cha kuzaliwa humpa mtoto haki za kurithi mali za wazazi wake. Alimalizia.

Mtu yeyote aliyezaliwa katika ardhi ya Tanzania Bara bila kujali umri ,jinsia au mahali anapoishi anastahili kupata cheti cha kuzaliwa .Hata hivyo ili mtu aweze kupata cheti hicho  anapaswa kuwa na kiambatisho kati ya vifuatavyo; Tangazo la kizazi kutoka kituo cha tiba alichozaliwa mtoto./ Kadi ya kliniki ya mtoto/ Cheti cha ubatizo/ Kadi ya kliniki ya mtoto/ Kadi ya kupiga kura pamoja na kadi ya uraia.

RITA inashiriki katika maonesho ya nanenane kitaifa mkoani Simiyu yaliyoanza tarehe moja mwezi huu hivyo inawasisitiza wananchi waliokaribu na viwanja vya nanenane kutembelea katika banda lao lililopo karibu na bustani ya Suma JKT ili kufaidika na huduma mbalimbali za Wakala ikiwemo kupata cheti cha kuzaliwa. Mgeni rasmi katika maonesho hayo alikuwa ni Mhe. Samia Suluhu.
  Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye misururu mirefu wakipata huduma ya vyeti vya kuzaliwa katika banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo katika maonesho ya nanenane mkoani Simiyu.
Afisa Usajili Msaidizi Bw. Haidary Malick(kulia) kutoka  RITA akikabidhi cheti cha kuzaliwa kwa Bw.Wenceslaus Boma mzaliwa wa Newala,Mtwara katika maonesho ya nanenane mkoani Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad