HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 1, 2019

PSPTB YATANGAZA RASMI MATOKEO YA 18 YA BODI HIYO

BODI ya wataalamu wa ununuzi na ugavi imeidhinisha matokeo ya 18, pamoja na kutangaza rasmi nafasi ya usajili kwa ajili ya mitihani ya 19 ya bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijiji Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa leo Julai mosi bodi ya wakurugenzi imeidhinisha rasmi matokeo ya bodi ya 18 na yameidhinisha kuwa rasmi.

Amesema kuwa mitihani hiyo ilifanywa katika vituo vitano nchini na zaidi ya watahiniwa 1400 walifanya na mtihani huo na watahiniwa zaidi ya 50 hawakuweza kufanya mitihani hiyo.

Aidha amesema kuwa Kuna baadhi ya watahiniwa ambao watarudia mitihani hiyo na kueleza kuwa masomo yanayojitaji hesabu nguvu kwa kuwa ufaulu bado ni hafifu hivyo ni somo ambalo linahitaji mkazo.

Vilevile amesema kuwa watahiniwa wawe na mawazo chanya na wao Kama bodi watasimamia  vigezo vya ufaulu na kueleza kuwa uhidhinishaji wa matokeo hayo yanafungua milango ya kukisajili kwa mitihani ya 19.

Aidha amesema kuwa kutakuwa na warsha maalumu pamoja na kuwatahini katika masuala ya kuandika tafiti na kujieleza kwa kuwa wanaandaa was kuwa viongozi wa baadaye.

Amesema kuwa ngazi zote za mafunzo zitazingatiwa na hiyo ni pamoja na kanuni na Sheria zote za mitihani huku akiwataka watahiniwa kuzingatia masomo ya hisabati.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya bodi ya 18, pamoja na kutangaza rasmi nafasi ya usajili kwa ajili ya mitihani ya 19 ya bodi hiyo itakayofanyika mwezi Novemba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad