HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 10, 2019

SPIKA WA BUNGE LA RWANDA ATEMBELEA BUNGE LA TANZANIA

  Spika wa Bunge,  Job Ndugai (kulia) akizungumza  na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille Ofisini kwake Jijini Dodoma mapema leo wakati Spika huyo wa Rwanda akiwa ameambatana na Wabunge wawili walipoanza ziara ya siku tatu ya kutembelea Bunge la Tanzania.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akimkaribisha Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille katika meza yake wakati alipomtembeza katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akimueleza jambo Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille wakati alipomkaribisha kukaa katika kiti chake cha Uspika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille ndani ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille pamoja na Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa ziara ya Spika huyo wa Rwanda katika Bunge la Tanzania.

   Spika wa Bunge (wapili kulia) akizungumza wakati wa kikao kati ya Wajumbe kutoka Bunge la Tanzania na Wajumbe kutoka Bunge la Rwanda wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mukabalisa Donatille (wa pili kushoto) Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akimkabidhi picha ya Jengo la Bunge Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille Ofisini kwake Jijini Dodoma. (PICHA NA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad