HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 20, 2019

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA TIMU YA TAIFA STARS NCHINI MISRI

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekutana jana na wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars katika kambi ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.

Katika mazungumzo na wachezaji hao Spika alifikisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwataka vijana hao kupambana kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa katika mashindano ya Afrika yanayotarajia kuanza Juni 21 nchini Misri.
Spika aliwataka wachezaji hao kuingia uwanjani wakiwa wamejua wamebeba matumaini makubwa kwa Watanzania ambao macho na masikio yao wameyaelekeza kwao.

Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alimuahidi Spika kuwa wamepokea salamu za  Rais Magufuli na wamemuahidi kuwa wataingia uwanjani kupambana na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya taifa.
Alisema hawataki kumuahidi kitu kikubwa,ila watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanapambana na kupata ushindani katika mechi zote za makundi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad