HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 17, 2019

Pwani, Simiyu watia fora fainali za mita 400 UMISSETA

Na Mathew Kwembe, Mtwara
Mikoa ya Pwani na Simiyu imeibuka vinara kwenye hatua ya fainali za mbio za mita 400 za mashindano ya  Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha ualimu Mtwara.

Mwanariadha Benedicto Mathias na mwenzake Amos Charles walijinyakulia medali za dhahabu na fedha kwa kushika nafasi ya kwanza na ya pili kwa upande wa wavulana huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mwanariadha Ismail Tosil kutoka mkoa wa Dar es salaam.

Mwanariadha Benedicto alitumia sekunde 51:30 kumaliza mbio hizo, na Amos alitumia sekunde 51: 50 huku Ismail wa Dar es salaam alitumia sekunde 52:48 kwenye mbio hizo za mita 400.

Kwa upande wa wasichana, medali ya dhahabu ilichukuliwa na mwanariadha Tereza Bernard kutoka Simiyu ambaye alitumia dakika 1:01:22, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Emmy Hosea wa Singida aliyetumia dakika 1:02:35 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Rahel Nila kutoka Simiyu aliyetumia dakika 1:03:34.

Katika mchezo wa mbio za kupokezana vijiti wavulana, hatua ya fainali 4 x 400 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mkoa wa Pwani ambao walifanikiwa kujinyakulia medali ya dhahabu baada ya washiriki wake wane kutumia jumla ya dakika 3:39:08 huku nafasi ya pili ikienda mkoa wa Mara ambapo washiriki wake walitumia jumla ya dakika 3:39:22 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mkoa wa Unguja ambapo washiriki wake wane walitumia dakika 3: 40:22.

Katika fainali za mbio za kupokezana  vijiti 4 x 400 nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mkoa wa Pwani ambao kwa pamoja wanariadha wake wanne walitumia dakika 4:16:36 na hivyo kuibuka nafasi ya kwanza, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mkoa wa Simiyu ambapo wanariadha wake walitumia jumla ya dakika 4:21:41 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mkoa wa Singida baada ya wanariadha wake wanne kutumia dakika 4: 25:41

Katika hatua ya fainali za mbio za kupokezana vijiti 4 x 100 kwa wavulana nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mkoa wa Dar es salaam, nafasi ya pili ilichukuliwa na Unguja na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mkoa Mara.

Mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo kulifanyika mbio za mita 100 kwa walimu,ambapo baadhi ya washiriki walitia fora kwenye mbio hizo kufuatia umahiri mkubwa waliouonyesha wa kukimbia licha ya umri wao mkubwa.

Mashindano ya UMISSETA yanatarajiwa kufungwa tarehe 21 juni, 2019 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako katika uwanja wa Nangwanda sijaona Mtwara.
Mshindi wa kwanza mbio za mita 400 Tereza Benard wa simiyu (mbele) akifuatiwa na mshindi wa pili Emmy Hosea kutoka Singida na nyuma yake ni Rahel Nila kutoka Simiyu mara baada ya kumaliza mbio za mita mia 400 leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
   Mshindi wa kwanza Benedicto Mathias kutoka Pwani, wa pili Amos Charles  na wa tatu Ismail Tosil wa Dar  wakimaliza mbio za mita 400 wavulana asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Baadhi ya wanariadha wa mbio za kupokezana vijiti kutoka mikoa iliyotinga hatua ya fainali wakipokea maelekezo kutoka kwa wasimamizi wa mchezo wa riadha kabla ya kuanza mbio hizo leo asubuhi katika viwanja vya chuo ncha ualimu Mtwara

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad