HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 26, 2019

MA -DC MKOANI PWANI WAAGIZWA KUANZA UTEKELEZAJI WA CHF ILIYOBORESHWA HADI IFIKAPO JULAI 31 -NDIKILO

 Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
SERIKALI mkoani Pwani,amewaagiza wakuu wa wilaya mkoani humo, kuhakikisha wanaanza utekelezaji wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF)kuanzia sasa na ifikapo Julai 31 mwaka huu apewe taarifa juu ya utekelezaji huo kwa halmashauri zote.

Aidha amewahamasisha wananchi ,kujiunga na CHF iliyoboreshwa kwa sh.30,000 kwa familia ya watu sita, badala ya 10,000 ya awali ili kupata matibabu kirahisi kwa kipindi cha mwaka mzima.
 Akizindua utekelezaji wa mfuko huo kwa mkoa wa Pwani, Miono Bagamoyo, mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza hataki kusikia visingizio hivyo ifikapo Julai 31 utekelezaji uanze kwa kila wilaya.

"Ila isiwe tena hamasa hii ikaachiwa kwa wakuu wa wilaya pekee kisa nimewaagiza hapana, hamasa hii ikafanyike kwa madiwani,maofisa tarafa,wenyeviti wa vijiji,kata,mitaa,watendaji na wadau waelimishe wananchi katika vijiji ,kata,tarafa na mitaa yao"alifafanua Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema, mikoa ya Shinyanga,Dodoma na Morogoro imeshafanikiwa sana hivyo na mkoa wa Pwani ni zamu ya kuhamasisha ili watu wajiunge kwa wingi .

"Kiwango hicho cha 30,000 ambacho ni kama 5,000 kwa kila mmoja kwa wanafamilia sita kitasaidia kutibiwa mwaka mmoja kuanzia ngazi ya zahanati,hospitali ya wilaya na hospitali ya mkoa badala ya zamani ambapo 10,000 ilikuwa ukitibiwa katika kituo na kijiji ulipo pekee" "Magonjwa hayapigi hodi tusiweke rehani maisha yetu kwa kuona 30,000 ni kubwa ,tulinde afya zetu ,alisema Ndikilo.

Ndikilo aliongeza, katika kukabiliana na changamoto zilizokuwepo kipindi cha nyuma na kuzingatia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015-2020 na mipango mkakati wa sekta ya afya 2015-2020 serikali imeweka mkakati ikiwemo kuongeza bajeti katika sekta ya afya hususan kwenye vifaa tiba na dawa.

"Kwa hili, sisi mkoa wa Pwani, bajeti yetu ni zaidi ya bilioni mbili tumepokea 2018-2019 kwajili ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha sekta hiyo'"aliweka bayana.

Pia ameelekeza, serikali ya kijiji cha Miono kata ya Miono Bagamoyo,kumthibitishia majina ya wajane na wagane wote waliopo katika kijiji hicho ili awalipie kujiunga na mfumo huo .

Awali meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) Mkoani Pwani,Ellentoruda Mbogoro aliwatoa shaka wananchi na kuwaomba wasikate tamaa kwani kwa sasa vifaa tiba na dawa zitakuwepo za kutosha katika vituo vya afya na hospital.

Mkazi wa kijiji cha Miono ,Fatma Mrisho alisema mpango huu ni mkombozi hasa kwa kaya zilizo na maisha duni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad