HAULE, BRAISON WAJIFUNGA AZAM FC - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 June 2019

HAULE, BRAISON WAJIFUNGA AZAM FC

NYOTA wawili wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kipa Benedict Haule na kiungo Braison Raphael, wameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kila mmoja wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Wawili hao ambao kila mmoja alikuwa akimaliza mkataba, wanatarajia kudumu kwa matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex hadi 2021.

Wachezaji hao kuongeza mkataba huo, ni muendelezo wa uongozi wa Azam FC chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', kwa kushirikiana na benchi la ufundi, linaloongozwa na Kocha Mkuu mpya, Etienne Ndayiragije, kuwabakisha nyota wenye umuhimu kikosini.

Nyota hao wanatarajia kuanza maandalizi ya msimu mpya na kikosi hicho Alhamisi hii, wakianza na changamoto ya kuiongoza timu hiyo kutetea ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame, itakayofanyika Rwanda Julai mwaka huu.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin 'Popat' akiwa anapeana mkono na kiungo Braison Raphael baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili na kuendelea kusalia katika klabu hiyo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin 'Popat' akiwa anapeana mkono na Golikipa Benedict Haule baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili na kuendelea kusalia katika klabu hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad