HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 18, 2019

Dar, Mwanza zatinga nusu fainali UMISSETA 2019 soka wasichana

Na Mathew Kwembe, Mtwara,
Timu za soka wasichana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Iringa na Ruvuma zimetinga hatua ya nusu fainali baada ya jana kufanikiwa kuwalaza wapinzani wao katika hatua ya robo fainali iliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa saa 8 mchana jana, timu ya soka ya wasichana ya mkoa wa Dar es salaam iliifunga timu ya mkoa wa Lindi kwa magoli 5 kwa 0, Iringa iliichapa timu ya Morogoro 3 kwa 1, Mwanza waliitoa Tabora kupitia mikwaju ya penati 3 kwa 2 baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja, huku Kilimanjaro pia nayo ilitolewa kwa penati 4 kwa 3 baada ya kutoka suluhu ya kutofungana ndani ya dakika 90 za mchezo.

Kufuatia matokeo hayo timu ya mkoa wa Dar es salaam wasichana itamenyana na Iringa katika hatua ya nusu fainali inayotarajiwa kuchezwa kesho  saa 2 asubuhi na kufuatiwa na mchezo mwingine wa nusu fainali ambao utawakutanisha Mwanza watakaochuana na Ruvuma.

Kwa upande wa mpira wa kikapu wasichana, mechi za robo fainali zilitarajiwa kuchezwa leo ambapo timu nane zilizotinga nusu fainali ni Morogoro ambayo itachuana na Singida, Dar es salaam wamepangwa kukutana na Dodoma, Mwanza wamepangwa kucheza na Tabora na Arusha watamenyana na jirani zao Kilimanjaro

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali na ambazo zinatarajiwa kuchuana leo kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana ni pamoja na timu kutoka mkoa wa Pwani ambao wamepangwa kucheza na Mbeya, Unguja watacheza na Arusha, Dar es salaam watachuana na Tanga na Morogoro wamepangwa kucheza na timu kutoka mkoa wa Shinyanga.

Washindi wa mechi za leo katika mpira wa kikapu kwa wavulana na wasichana wanatarajiwa kucheza kesho katika hatua ya nusu fainali ambapo mechi za kutafuta mshindi wa tatu na fainali zenyewe zinatarajiwa kuchezwa tarehe 21 juni, 2019.
Wachezaji wa timu ya soka wasichana kutoka mkoa wa Kilimanjaro wakipambana na wapinzani wao timu ya soka wasichana ya mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad