HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 10, 2019

StarTimes watembelea Shule ya Msingi Taifa kuitambulisha ST Kids

StarTimes Tanzania imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. 

Siku ya Ijumaa walitembelea shule ya Msingi Taifa iliyoko Temeke jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 4 na 5 katika shule hiyo.

Mbali na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi cha Dish kwa uongozi wa shule na zawadi kadha wa kadha kwa wanafunzi waliojibu vizuri maswali na wale wanaofanya vizuri darasani.

“Ugeni wenu umewapatia wanafunzi chachu ya kujifunza Zaidi kwani kama tunavyojua watoto wanapenda hujifunza Zaidi kwa kutazama kuliko kusikiliza. Lakini pia imetusaidia kujua wapi kuna tatizo na sisi tunaweza kuongeza nguvu katika kuwafundisha wanafunzi wetu,” alisema Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Taifa Bi. Juliana Lubuva.

“Lakini pia tuwapatie changamoto StarTimes wongeze maudhui ya teknolojia Zaidi kupitia katuni kwa sababu watoto wanaelewa Zaidi itawpa msukumo wa kupenda masomo ya sayansi na kupanua uelewa wao.” Aliongeza. 

ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.

“Tunapotembelea shule hizi tunakuwa na vipengele vitatu ambavyo ni, maswali kwa wanafunzi wanaoongoza darasani, maswali kwa wanafunzi wote na kasha kuangalia katuni na maswali juu ya wahusika wa katuni an mafunzo yanayopatikana katika katuni.” Zamaradi Nzowa Meneja Maudhui, StarTimes Tanzania.
Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam.

Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
 Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa(kushoto) akimkabidhi dishi na Dekoda la Startimes Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Taifa, Juliana Lubuva(kulia) wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. 
 Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa akizungumza na  baadhi ya wanafunzi wa darasa la 3 , 4, 5 na la 6  wa shule ya Msingi Taifa iliyoko Temeke  wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
 Wanafunzi wa darasa la 3 , 4, 5 na la 6  wa Shule ya Msingi Taifa iliyoo Temeke jijini Dar es Salaam wakiangalia katuni zinazopatikana kwenye chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
 Baadhi ya wanafunzi waliojinyakulia zawadi wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wao pamoja na wafanyazi wa Startimes Tanzania
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Taifa, Juliana Lubuva akitoa shukrani kwa Startimes Tanzania kwa kuweza kuwakumbuka wakati wa kukabidhiwa zawadi ya King'amuzi cha Startimes wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya kutambulishwa kwa maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili katika Shule ya Msingi Taifa iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad