HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 14, 2019

StarTimes waipeleka ST Kids Swahili Shule ya Msingi Tabata

Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. 

Jumanne hii walitembelea shule ya Msingi Tabata iiliyoko Ilala jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 2, 3, 4 na 5 kutoka shule hiyo.

Pamoja na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi na Dish kwa uongozi wa shule na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi walioweza kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa.

“Tumepokea vizuri ugeni wa StarTimes hapa shuleni kwetu na kwa zawadi waliyotupatia. Pia wamewapatia changamoto nzuri wanafunzi wetu kwa maswali waliyowauliza.” Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Tabata Bi. Rosalia P. Mrema.

ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.
“Lengo letu kutembelea shule hizi ni kutambulisha maudhui mapya yanayopatikana katika chaneli ya ST Kids ambayo yako katika lugha ya Kiswahili.

Vipindi ni vizuri kwa watoto kwani vinawafundisha stadi mbali mbali za maisha na pia vinaleta uhusiano mzuri baina yao na wazazi kwani wanaweza kuelezea hisia zao kupitia vipindi hivyo” Samwel Gisayi - Afisa Mahusiano, StarTimes Tanzania.
Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano na itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam.

Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
 Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kushoto) akimkabidhi zawadi ya dekodam ya Startimes Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tabata Rosalia P. Mrema wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
 Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa(kulia) pamoja na Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios wakimwonesha vifaa mbalimbali vinanyotumika kwenye king'amuzi cha Startimes  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tabata Rosalia P. Mrema(katikati) wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili katika shule hiyo leo.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad