HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 14, 2019

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUONGEZA KASI YA UFUGAJI SAMAKI

*Wastani wa mtu mmoja kwa mwaka ni kula samaki kilogram 20.

Na Chalila Kibuda  Michuzi TV
Serikali imesema kutokana kuwapo kwa uhaba wa samaki nchini imeweka mikakati ya kuongeza kasi ya ufugaji wa samaki hao kwa ajili ya kutosheleza katika soko la ndani na nje ya nchi.

 Kwa wastani mtu mmoja anatakiwa kula samaki Kilogramu 20 kwa mwaka, lakini nchini mtu mmoja anakula Kilogramu 7.9  kwa mwaka wakati samaki ana virutubisho vingi katika mwili wa binadamu.

 Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Utunzaji Viumbe Maji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Nazael Madala, wakati akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau wa viumbe hai wakiwamo watafiti, wafugaji na wanafunzi kwa lengo la kijadili namna ya kuboresha sekta hiyo na umuhimu wa sekta binafsi katika kuwekeza katika uzalishaji wa samaki ardhini.

“Nchini tani 350,000 hadi 380,000 za samaki zinazalishwa kwa mwaka ambazo hazitoshelezi kulingana na mahitaji yaliyopo na kukabiliana na  na uhaba  wizara inahimiza wavuvi na wadau wengine kujikita kwenye ufugaji wa samaki," amesema Dk. Madala.

 Amesema kupungua kwa samaki kunatokana na  kuwepo kwa uvuvi haramu, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi na kufanya samaki kupungua  kwa zaidi ya miaka 20 bila kuongezeka. .

 Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Wakuzaji wa Viumbe Maji Tanzania(AAT),Geoffrey Rucho, amesema  lengo la mkutano huo ni kuhakikisha utafiti uliofanywa kuhusu hali halisi ya viumbe hai nchini na kuwakutanisha wadau kujadili kutaleta  mabadiliko chanya katika sekta hiyo kwa kuongeza uzalishaji wa samaki na kufikia malengo ya wizara.

 Naye Mtaalamu wa viumbe hai, Profesa  Philip Bwathondi, alisema viumbe hao wa majini kama samaki wamepungua kwa sababu watumiaji wameongezeka na vifaa vya kuvulia vimeongezeka.

Amesema njia ya kuongeza viumbe hao ni kuanza kufuga na kusaidia wavuvi wengine kujikita kwenye kufuga na kuongeza uzalishaji.

Bwathondi Amesema njia nyingine ni kufuga samaki wadogo ambao wakifika umri wa ukuaji wanamwagwa kwenye eneo moja la ukuaji ili kupunguza upungufu uliopo,  kwani kuna tofauti ya samaki wa baharini na wakufungwa, wale wanaofugwa ni wazuri zaidi kwa sababu wanapewa vyakula bora.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ukuzaji Viumbe Wizara ya Mifugo , Uvuvi Kajitanus Osewe akichangia mada kwenye mkutano wa viumbe hai wakiwamo watafiti, wafugaji na wanafunzi kwa lengo la kijadili namna ya kuboresha sekta hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Wadau wakiwa katika mkutano wa wadau wa viumbe hai wakiwamo watafiti, wafugaji na wanafunzi kwa lengo la kijadili namna ya kuboresha sekta hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja  ya pamoja ya wadau wa wadau wa viumbe hai wakiwamo watafiti, wafugaji na wanafunzi kwa lengo la kijadili namna ya kuboresha sekta hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ukuaji wa Viumbe Hai wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Nazael Midala akizungumza na waandishi katika mkutano wa wadau wa samaki uliofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad