HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 8, 2019

STARTIMES YAENEZA MAUDHUI YA WATOTO KATIKA SHULE DAR

KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Jana Mei 7, wawakilishi wa kampuni hiyo wametembelea ya Shule ya Msingi Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 3 na 4 kutoka shule hiyo pamoja na  kutoa zawadi  ya king’amuzi cha Dish kwa uongozi wa shule na zawadi kadha wa kadha kwa wanafunzi waliojibu vizuri maswali na wale wanaofanya vizuri darasani.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea wageni hao mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo Amani Levison amesema kuwa, “Tunashukuru sana kwa ugeni huu wa StarTimes kwa kuja shuleni kuzungumza na wanafunzi na kuwapatia chachu ya kujifunza zaidi na kuwasaidia kupata msukumo wa kufanikiwa kwenye masomo yao” amesema.

Amesema, "Pia maudhui ya chaneli hii yamewachangamsha wanafunzi na itakuwa ni sehemu ya ukuaji wao kwa sababu kuna vitu vingi wanavyoweza kujifunza kupitia vipindi ambavyo vinafundisha sanaa na stadi mbali mbali za kimaisha.” Ameongeza.

ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, huku lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambay wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.


Kwa upande wake meneja maudhui wa Startimes Zamaradi Nzowa amesema kuwa vipindi vingi vina mafunzo ya ustadi ambao utawasaidia watoto kujijijenga kiakili na kujiamini zaidi na  lengo lao shuleni happ ni kuja shule hapo ni kwa sababu wanafunzi wa shule hiyo wanabeba uhalisia wa watoto wengi wa kitanzania.

Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios akiuliza maswali na kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala(katikati) akitoa shukrani kwa Startimes Tanzania kwa kuweza kuwakumbuka wakati wa kukabidhiwa zawadi ya King'amuzi cha Startimes wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. Kulia ni Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa na kushoto ni Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kulia) akimkabidhi zawadi ya dishi la Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. Kulia ni Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa.
Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa(kushoto) akimkabidhi dekoda ya Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala(kulia) wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. 
Wanafunzi wa darasa la 3 na 4 kutoka shule ya msingi Mchikichini wakiangalia iliyoko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam wakiangalia katuni zinazopatikana kwenye chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad