HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 8 May 2019

MILIONI 700 ZA RAIS MAGUFULI ZAANZA KUTOA MATOKEO POLISI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akipita kukagua ujenzi wa majengo mapya na ya kisasa yanayojengwa katika Chuo cha Maofisa wa Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es salaam, ujenzi unaotokana na fedha iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kiasi cha shilingi milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa Chuo hicho cha Maofisa. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akifurahia jambo huku akiwa amembeba mtoto aliyefika katika hospitali Kuu ya Polisi iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam leo, akiwa na mzazi wake kwa ajili ya kupata huduma za matibabu hospitalini hapo, IGP Sirro amefanya ziara ya ghafla ya ukaguzi yenye lengo la kuona namna huduma za matibabu zinavyotolewa pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na Maofisa wa Polisi  wanaofanyakazi katika hospitali Kuu ya Polisi iliyopo Kurasini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya ghafla ya ukaguzi yenye lengo la kuona namna huduma za matibabu zinavyotolewa pamoja na changamoto wanazokutananazo ambapo IGP Sirro amewataka viongozi hao kutoa huduma bora kwa wateja.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu  Dkt. C. Msenga wa hospitali ya Jeshi hilo iliyopo Kurasini Jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya ghafla ya ukaguzi hospitalini hapo. Picha na Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad