NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Suleiman
Jafo amezindua vyumba vya madarasa matatu, katika shule ya msingi
Masanganya ,kata ya Kibuta, wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Akizindua madarasa hayo ambayo yamejengwa na mkandarasi anayejenga
reli ya kisasa SGR kupitia kampuni ya Yapi Merkezi kwa kushirikiana na
Shirika la Reli Tanzania (TRC ) ,ameipongeza kampuni hiyo kwa kujenga
madarasa hayo na kukarabati vyumba vingine vitano vya madarasa.
Jafo ,aliyataka makampuni mengine yaliyowekeza mkoani humo kuiga mfano
uliofanywa na Yapi Merkezi kwa kupitia TRC kwani mkoa bado una
changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elimu .
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza, mkoa huo
bado unakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa vyumba vya
madarasa 3,600.
Ndikilo, aliwataka walimu na wanafunzi kutunza miundombinu hiyo ili
iweze kudumu kwa kipindi kirefu.

Akitolea ufafanuzi, hali ya kielimu kimkoa, alibainisha kwamba
inazidi kuimarika kwani matokeo ya darasa la la saba kwa mwaka 2017
mkoa ulishika nafasi ya 19 kati ya mikoa 26 na kwa mwaka 2018 mkoa
ulishika nafasi ya 11.
No comments:
Post a Comment