HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 5 May 2019

BASI LA KILIMANJARO EXPRESS LAPINDUKA MKATA,LILIKUWA LIKITOKA ARUSHA KWENDA DAR

 Basi la Kilimanjaro lenye namba za usajili  T 983 AWY limepinduka jioni ya leo mbele ya eneo la MKATA, Tanga. Basi hilo lilikuwa likitokea  Arusha kuelekea jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wameeleza kuwa katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha eneo la tukio zaidi ya majeruhi kadhaa,Wakielezea zaidi mbele ye Michuzi TV kuhusu chanzo cha ajali hiyo,wakabainisha kuwa chanzo ni mwendo kasi wa basi hilo.

Tutawaletea zaidi  taarifa kamili kutoka Mamlaka husika.
Baadhi ya Abiria waakiangalia baadhi ya majeruhi na ukaguzi wa mizigo yao kufuatia basi hilo kupinduka maeneo ya Mkata,likiwa linatoka  Mkoani Arusha kuelekea jijini Arusha.
Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wakitoa msaada kwa majeruhi
Baadhi ya Abiria waakiangalia baadhi ya majeruhi na ukaguzi wa mizigo yao kufuatia basi hilo kupinduka maeneo ya Mkata,likiwa linatoka  Mkoani Arusha kuelekea jijini Arusha.
Basi la Kilimanjaro lenye namba za usajili T 983 AWY likiwa limepinduka mbele ya eneo la MKATA, Tanga,hakuna aliyepoteza Maisha.


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad