HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 23, 2019

WATER HEALTH YAADHIMISHA SIKU YA MAJI KWA KUWATAKA WANAFUNZI KUWA MABALOZI BORA KATIKA SEKTA HIYO

IKIWA ni kilele cha maadhimisho ya siku ya maji duniani leo Machi 22 muanzilishi wa taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health)Diana Kato ametoa elimu ya maji safi na salama na matumizi yake katika shule tatu za jiji la Dar es salaam ambazo ni shule za msingi Mtambani, Tabata na Tabata Jica.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Kato amewataka wanafunzi huo kuwa mabalozi bora katika kutunza vyanzo vya maji bila kuvichafua wala kuruhusu watu wengine wavichafue vyanzo hivyo kwa namna yoyote ile.

Aidha amesema kuwa kampeni kuhusiana na sekta ya maji ni endelevu kwani umuhimu wake ni mkubwa sana na kueleza kuwa elimu zaidi inahitajika ili kukomesha tabia ya uharibifu wa mazingira unaochangia kuhatarisha sekta hiyo.

Katika maadhimisho hayo elimu ilitolewa kupitia mabango yanayoeleza umuhimu na faida za maji pamoja na kuulizwa maswali na walimu wao kuhusiana na sekta nzima ya maji.

Pia Kati amekabidhi vitabu kwa shule hizo vilivyotolewa na Nyambari Nyangwine Publishers ambavyo vitawasaidia katika kujifunza na kuongeza maarifa zaidi.
 Muanzilishi wa Taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health) Diana Kato akizungumza na wanafunzi wa shule ya shule za msingi Mtambani, Tabata na Tabata Jica wakati wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.

Mwalimu mkuu wa shule za msingi ya Tabata, Khamis Ngoda  akizungumza na wadau wa maji pamoja na wanafunzi wa shule za msingi Mtambani, Tabata na Tabata Jica wakati wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.
 Mmoja wa wafafuzi akitoa shukrani kwa uongozi wa Taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health) baada ya kupokea zawadi ya vitabu wakati wa wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.
  

Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye picha za pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya vitabu kutoka Taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health)  wakati wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad