HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 26, 2019

MCHAKATO WA AWALI WA KUPATA TIMU 32 ZA KUSHIRIKI MASHINDANO YA SOKA YA MSIMU WA PILI YA ‘CASTLE LAGER 5s ASIDE KUKAMILIA WIKI HII

Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitaa bia yake ya Castle Lager kwa mara nyingine tena imekuja na mashindano ya “Castle Lager 5s Aside”(wachezaji watano watano kila upande) msimu wa pili jijini Dar es Salaam utakaoshirikisha takribani Bar 60 za jiji la Dar es Salam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alisema tayari mchakato wa kutafuta timu shiriki za fainali za mashindano hayo kupitia timu za promosheni kwenye Bar mbalimbali za jijini Dar es Salaam umeshaanza na tayari Bar 48 tumeshazifikiwa ambapo wiki hii tunatarajia kuzifikia tena Bar 12 kukamilisha Bar 60 kwa raundi ya kwanza.

Tutarudi tena kwa raundi ya pili katika hizo Bar kuhakiki timu zao na Bar 32 zitakazokuwa zimeongoza kwa mauzo zitakuwa zimefuzu rasmi kuingia kwenye fainali ya Bonanza kubwa litakayofanyika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam alisema Kikuli. Aidha Kikuli aliwashukuru wakazi wa jijini Dar es Salaam kwa kuitikia wito kwani mwamko wa mwaka huu ni mkubwa ukilinganisha na mwaka jana kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam, kwani kila Bar miongoni mwa Bar 60 zilizoingia kwenye mchakato zinashauku ya kutaka kushiriki mashindano hayo.

Mashindano haya yanafanyika hapa nchini kwa mara ya pili, chini ya udhamini wa Bia ya Castle Lager. Hata hivyo yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika. Mwaka jana tuliyafanya kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika michuano ya Kimataifa ya Afrika, iliyofanyika nchini Zambia kwa kuzikutanisha timu za Afrika Kusini, Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia.  

Mwaka huu, tunatarajia kuwa na mashindano bora zaidi yatakayotusaidia kupata washindani na mabalozi wazuri katika michuano ya kimataifa. Mchakato wa kupata timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo umeboreshwa zaidi mwaka huu, ambapo washiriki watapatikana kupitia katika promosheni zitakazofanyika katika baa mbalimbali jijini Dar es Salaam. Lengo ni kuwafikia wanywaji wa bia ya Castle Lager ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa ya kutimiza ndoto zao.
Timu zetu za promosheni zimekuwa zikipita baa mbalimbalia kwaajili ya kutoa maelekezo kwa wateja kwa namna ambayo wanaweza kushiriki katika uundaji wa timu zao. 

Ili kuingia 32 bora, moja ya kigezo muhimu ni kufanya mauzo mengi ambapo kutakuwa na makasha maalumu katika baa husika kwaajili ya kukusanyia vizibo baada ya mteja kununua bia ya Castle Lager. Niwaombe watanzania kutumia nafasi hii, ambayo itawapa wakati mzuri wa kutimiza ndoto zao. Wakati mwingine fursa kama hizi ni nadra sana kutokea.

Castle Lager tunaendelea kuwapa kile kilicho bora wateja wetu, ikiwa ni pamoja na kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwamo kukuza na kutoa fursa kwa wenye vipaji vya michezo.
Mwisho, Nirudie kusisitiza kwamba, michuano ya Castle Lager 5- Aside ina nafasi kubwa ya kuitangaza nchi yetu, na kutangaza vipaji binafsi kwasababu inafanyika hadi ngazi ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad