HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 26, 2019

HDIF yakutanisha wadau wa sekta ya afya kujadili fursa na vikwazo katika kutumia tehama kwenye kukuza sekta ya afya

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MFUMO  wa teknolojia kwenye sekta ya afya utasaidia kupunguza matumizi ya makaratasi ambayo huchelewesha wagonjwa kupata huduma.

Hayo yamebainishwa leo Machi 26, 2019 na Mkurugenzi wa Ufundi wa Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya watu (HDIFl) Muzafar Kaemdin wakati wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu yaliyoandaliwa na HDIF kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech).

Amesema matumizi ya makaratasi wakati wa uchukuaji taarifa za wagonjwa hutumia muda mrefu kuliko kutoa huduma husika hivyo matumizi ya Tehama yatachochea utoaji wa huduma bora za afya kwa wakati.

"Tumewakutanisha wadau wa afya pamoja na serikali na tulichojifunza ni wadau wa maendeleo kuhakikisha wanajua ni watu gani wa kuwasiliana nao ili kuanzisha mifumo ambayo haikuwahi kuanzishwa ili kusaidia kutoa huduma za afya na sio kila mdau kuwa na miradi  inayofanana nchini ambapo kufanya hivyo kutasaidia hivyo ni muhimu kuwasiliana na serikali kabla
ya kuanzisha miradi," alieleza Kaemdin.

 Kwa upande wake, Ofisa Tehama kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sultana Seif akiwasilisha mada,kuhusu hali ya utumiaji wa Tehama katika sekta ya afya amesema, utumiaji wa Teknolojia  Habari na Mawasiliano (Tehama), katika sekta ya afya  imekuwa na kufikia asilimia 70 ambayo imesaidia kurahisisha utoaji wa huduma bora katika vituo vya afya na hospitali nchini.

Amesema, pia mfumo hwa Tehama wa E-health unasaidia kufuatilia utoaji wa chanjo kwa watoto unaowawezeaha kutambua siku aliyozaliwa, chanjo alizopata na zile ambazo hakuzipata ili kuhamasisha  was a so kuwapeleka watoto wao kliniki kupata chanjo husika kwa ajili ya kuwakinga na magonjwa.

Seif amesema, kuwa mfumo huo ambao umeisha anza kutumika umeleta matokeo chanya kwa kuwa sasa mtu unauwezo wa kufuatilia upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba kwenye hospitali na vituo vya afya mijini na vijijini.

"Mfumo huu ulipoanza kutumika, mwaka 2015, watumishi wengi wa sekta hii ya afya hawakuukubali kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha lakini kutokana na mafunzo mbalimbali, wameukubali na sasa unatumika bila matatizo", amesema.

Amesema malengo makubwa ya mfumo huo wa E-health ni kusaidia taarifa kufikia vituo vya afya vilivyopo vijijini na  kutoa huduma bora kwa wakati.

Ameongeza kuwa, serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa sekta ya afya inatolewa kwa njia ya kidijitali ili kuboresha huduma hizo kwani kila mwananchi ana haki ya kupata huduma bora za  na ndio maana serikaki ikatafuta namna bora ya kuboresha huduma hizo na  kuzingatia usiri na usalama wa taarifa za wateja wetu.

Pia alisema wadau wa maendeleo na taasisi nyingine za serikali zimeshiriki kutengeneza mfumo huo kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa kuandaa mazingira ya usawa na haki.

Alieleza miongozo hiyo inasaidia wadau kufanya kazi kwa kufuata miongozo iliyowekwa kwa sababu kumekuwa na changamoto ya wadau wa maendeleo kuanzisha miradi ya afya na kisha kuiacha bila kuiendeleza hivyo hupoteza rasilimali na haileti manufaa.

Naye,ll Meneja Program wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana kutoka Shirika la  Amref, Dk Serafina Mkua amesema serikali imefanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya afya kwa njia ya kidijiti na sasa  inalekea kuondoka kwenye data ambazo zinakusanywa kupitia makaratasi na kwenda kwenye mfumo huo wa  E-health ambapo sasa watatumia simu na  kompyuta kukusanya taarifa.

"Miongozo ambayo imewekwa ni kitu kizuri ambacho kitasaidia wadau wote katika kutekeleza mikakati ambayo ipo lakini pia  kuleta bunifu zinazofuata miongozo ambayo ipo tayari.  Itasaidia  kuboresha utendaji lakini pia utoaji wa huduma kutokana na mabadiliko hayo," alisema Dk Mkua.
 Mkurugenzi wa Ufundi wa HDIF, Muzafar Kaemdin(kulia) akiongoza mjadala wa umuhimu wa matumizi ya Huduma bora za afya  kwa kutumia Teknohama. Uliohudhuriwa na wataalamu wa maendeleo ya afya wakati Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
 Meneja Program wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana kutoka Shirika la  Amref, Dk Serafina Mkua akizungumza na wataalamubwa afya namna serikali ilivyofanya  mabadiliko makubwa kwenye sekta ya afya kwa kitumia njia ya kidijitali wakati wa wiki ya ubunifu iliyoandaliwa na HIDF kwa kushirikiana na COSTECH.
 Ofisa Tehama kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sultana Seif(katikati) akiwasilisha mada kuhusu hali ya utumiaji wa Tehama katika sekta ya afya kwenye Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech).
Mjadala ukiendelea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad