HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 26, 2019

KTO YATOA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAKUFUNZI WA VYUO KUMI VYA MAENDELEO YA WANANCHI NCHINI

Na Francis Daudi, Blogu ya Jamii
WARSHA wa Mafunzo ya Siku Mbili katika kuwajengea Uwezo wakufunzi kutoka Vyuo kumi vya Maendeleo ya Wananchi vilivyoingizwa kwenye mradi wa Elimu Haina Mwisho unaohusisha vyuo  20 vya Maendeleo ya Wananchi kati ya 54 vilivyopo nchini. 

Mafunzo hayo yaliandaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) yamehitimishwa Leo huku wawezeshwaji wakishukuru kwa kupata fursa hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo,  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa ameeleza kuwa hiyo ni moja ya jitihada ya kuunga mkono juhudi za Serikali hasa katika kuwajengea Maarifa Wakufunzi na kwamba miradi ya namna hiyo ni sehemu ya mipango ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi kwa kuwa Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vina nafasi kubwa katika kulipeleka taifa katika uchumi wa viwanda.

Aidha, Ameongeza kwamba, Mfumo usio rasmi utawanufaisha Wanawake Vijana waliokatizwa masomo kutokana na sababu mbalimbali kama vile Kukimbia Ndoa za Utotoni, Ukeketaji na Ujauzito. Na hivyo basi mradi huo una malengo ya kuchangia katika jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwenye kuviimarisha Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi ili viwe na  tija kubwa kwa Wanawake vijana wengi wenye kutokea kwenye familia za  watanzania wenye vipato duni.  

Baadhi ya miradi ambayo taasisi ya KTO inashirikiana na wizara ni pamoja na ‘Elimu Haina Mwisho’ ambayo ni programu ya kuwapatia maarifa na ujuzi wanawake vijana waliokosa fursa  hiyo  kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni, ukeketaji na kupata ujauzito wakiwa shuleni. Vilevile, KTO inaendesha programu ya ‘ Mpira Fursa’ inayohusika na kuendeleza mpira kwa wanawake na hapa nchini mafunzo hutolewa katika Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi na Wanawake vijana wanaopata programu ya Mpira Fursa ambao hawajifunzi kucheza mpira pekee, bali pia kupata mafunzo na ujuzi mwingine.

Kwa muda mrefu KTO imekuwa kiungo muhimu katika Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi nchini na Wizara pamoja na wahisani wa Kimaendeleo kama SIDA,( Sweden) HDIF ( Uingereza) na Mastercard Foundation ( Canada) na wengineo wamekuwa bega kwa bega na KTO pamoja na kushiriki katika kuboresha utolewaji wa Mafunzo ndani ya Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi.


Akifunga Mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KTO,  Aidan Mchawa, Ameishukuru Serikali kwa kutoa nafasi ya kufanyika kwa Mafunzo hayo, amewasihi wakufunzi toka vyuo kumi vilivyoshiriki kutumia maarifa  waliyoyapata, ili yawe sehemu muhimu katika kuandaa Wanawake Vijana ambao kwa miaka ijayo ndio hasa watakuwa nguvu kazi ya Taifa.

Pia amelishukuru Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kuwezesha Warsha Mafunzo hii ya siku mbili.

Mafunzo hayo ya siku mbili, yalitanguliwa na Mafunzo ya siku kumi yaliohusisha vyuo 20, wakati huo taasisi ilitoa vifaa ambavyo vitawasaidia wawezeshwaji katika kutekeleza majukumu yao. Vifaa  hivyo ni pamoja na kompyuta 10 zenye thamani ya shilingi milioni 7, External hard driver 10 ambazo zina programu za kufundishia watoto kama vile Ubongo kids zenye thamani ya shilingi milioni 2.8, projector 20 zenye thamani ya shilingi milioni 18  pamoja na vitabu vya elimu ya awali vyenye thamni ya shilingi milioni 5.2.

Mafunzo hayo pia  yaliambatana pia na utolewaji wa Komputa  30 na Projekta 10 kwa Vyuo 10(Komputa 3 na Projekta 1 kila Chuo) vilivyotoa ushiriki wao katika Warsha hii ili vikasaidie utekelezaji wa mradi kwa Ufanisi.
Baadhi ya washiriki wa warsha huo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kupata mafunzo hayo, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya KTO Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa utolewaji wa mafunzo hayo ambapo amewataka wawezeshwaji kutumia maarifa waliyoyapata katika kuleta matokeo chanja katika jamii, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi KTO Aidan Mchawa akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ambapo ameishukuru serikali kwa ushirikiano na kuhaidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuendeleza taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad