HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 March 2019

DKT. MWANJELWA ATEMBELEA TAGLA, AWAPONGEZA KWA KASI KAZI NZURI

* Awataka kujitangaza zaidi ili wananchi waweze kujua kazi wanazozifanya, azungumza na chuo cha serikali cha nchini Kenya na wafanyakazi wa utumishi jijini Dodoma kupitia daraja video (video conference)

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NAIBU Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora Dkt. Mary Mwanjelwa ametembelea ofisi za wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini (TaGLA) huku akitoa pongezi kwa wafanyakazi kwa kazi hiyo wanayoifanya ambayo ni tofauti na yenye tija kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kutembelea vitengo vya wakala hiyo Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa kazi zinazofanywa na wakala hiyo zina tija kwa wananchi na Serikali na kuwataka kujitangaza zaidi ili wananchi waelewe majukumu yanayofanywa na wakala hiyo.

Aidha amewataka wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuzidi kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt.John Joseph Magufuli.

Amesema kuwa wizara anayoisamia ipo tayari kushirikiana nao  katika shughuli zao ambazo nyingi zimelenga kuokoa gharama za Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa wakala hiyo Charles Senkondo amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa wakala hiyo miaka 18 iliyopita wamekuwa na jukwaa la TEHAMA linalohusisha wanajamii mbalimbali.

Senkondo amesema kuwa majukumu ya wakala hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma na sekta binafsi kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia ikiwemo video Conference ambayo huwakutanisha watu tofauti kwa wakati mmoja hali inayopelekea kupunguza gharama.

Senkondo amesema kuwa  wakala hiyo pia inatoa huduma za mikutano ya kazi na zile za daraja video, midahalo huduma za maabara ya kompyuta.

Amesema kuwa wamejipanga katika kuhakikisha huduma hiyo inafika katika Mikoa yote nchini na tayari wamewasiliana na wizara ya mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa katika kushirikiana na sekta mbalimbali zikiwemo TANTRADE, TIC na madaktari bingwa katika kuwajengea uwezo.

Aidha amesema kuwa wana malengo ya kutoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA na kuendesha vikao vya kazi kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi ili kuwajengea uwezo na kuwafikia wafanyakazi hao kwa muda mfupi na kuokoa gharama.

Vilevile Senkondo amesema kuwa wamefanya midahalo mingi na nchi nyingine  zikiwemo Korea kusini na kenya na kujadili masuala mbalimbali ya kijamii kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na ukuaji wa miji kupitia mfumo wa daraja video huku akimpongeza Naibu waziri wa Viwanda na biashara Mhandisi Stella Manyanya kuwa balozi bora wa wakala hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo akieleza majukumu ya wakala hiyo mbele wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa mara baada ya kukagua utendaji kazi unaofanywa na wakala hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na watumishi mara baada ya Mkurugenzi mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo kuwasilisha majukumu ya wakala hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Meneja mafunzo na habari kutoka wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA Dickson Mwanyika akitoa mwongozo katika warsha hiyo iliyofanyika katika ofisi za wakala hiyo, leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na watumishi wa ofisi yake jijini Dodoma leo alipotembelea ofisi za TaGla leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA  wakiwa kwenye mkutano na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa alipotembelea ofisihizo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na wafanyakazi wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA mara baada ya kukagua utendaji kazi unaofanywa na wakala hiyo huku akieleza kufurahishwa na utendaji kazi wao, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akionesha zawadi aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa wakala hiyo Charles Senkondo, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa katika picha  ya pamoja na wafanyakazi wa TaGLA leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad