HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 15 February 2019

Wateja wa StarTimes walivyosherehekea Valentine’s Day

Siku ya tarehe 14 mwezi wa pili  husherehekewa duniani kote kama Siku ya wapendanao, kwa kiingereza Valentine’s Day. Hapa nchini pia siku hiyo inasherehekewa kwa watu kuwanunulia zawadi, kuwatumia jumbe wawapendao ama kwenda maeneo ya kupumzika na migawa ya chakula ikiwa ili kuwakumbusha kwamba wanawapenda.

Kwa upande wa Kampuni ya StarTimes wao waliandaa changamoto kupitia mitandao yao ya kijamii changamoto iliyoahamika kama #StarTimes10yearsCoupleChallenge ambapo wateja wao walitakiwa kuweka picha kwenye akaunti zao wakionyesha walikuwa wapi miaka 10 iliyopita na sasa wakiwa na wapenzi wao.

Siku ya tarehe 13 Jumatano kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii waliwatangaza washindi wawili wa changamoto hiyo ambao siku ya tarehe 14 walizawadiwa kupumzika katika hoteli ya kifahari ya Slipway iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam. StarTimes wakigharamia malazi, usafiri pamoja na chakula katika hoteli hiyo iliyoko Ufukweni mwa bahari.

“Tumekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 12 sasa mimi na mke wangu, hatujawahi kuwa na Valentine nzuri na ya kipekee kama ya mwaka huu. Kwa kweli tunawashukuru sana StarTimes kwa kutujali wao katika siku muhimu kama hii, tumefurahi sana” Jumanne James Mdoe, mmoja wa washindi.
Mbali na zawadi ya mapumziko katika hoteli hiyo StarTimes wametoa zawadi kwa washindi wengine 10 ambao wao watapata vifurushi vya mwezi mzima kwa kila mmoja. Majina ya washindi yanaendelea kutangazwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya StarTimes, Instagram pamoja na Facebook.
 Mshindi wa #StarTimes10yearsCoupleChallengLucas Robert akiwa na mwenziwe Catherine Marco ambao siku ya tarehe 14 walizawadiwa kupumzika katika hoteli ya kifahari ya Slipway iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam. 
Mshindi wa #StarTimes10yearsCoupleChallengLilian Lucas akiwa na mumewe Jumanne Mdoe ambao siku ya tarehe 14 walizawadiwa kupumzika katika hoteli ya kifahari ya Slipway iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad