HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 15, 2019

Milioni 7.5 yakabidhiwa kwa washindi 12 wa Promosheni ya Tusua Ada na Omo

Mkurugenzi Mkuu wa Uniliver Tanzania David Minja(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya mwisho, Nsalu Mbaga(miaka 29) mkazi wa Ubungo River side jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi milioni moja(1,000,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” iliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Supermarket ya Game Mlimani City.
Mkurugenzi Mkuu wa Uniliver Tanzania David Minja(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya mwisho, Angel Nyange(miaka 23) mkazi wa Kimara Mbezi jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi milioni moja(1,000,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” iliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Supermarket ya Choppies Mlimani City.

WAKAZI kumi na mbili wa jijini Dar es Salaam wafanyao manunuzi katika Supermarket za Game,Choppies Mlimani City na Shoppers Mikocheni,Masaki na Mbezi wamejishindia jumla ya shilingi milioni saba na nusu(7,500 000) ikiwa ni shilingi laki tano(500,000/=) kila mmoja katika wiki tatu mfululizo na wiki ya nne washindi watatu shilingi milioni moja kila mmoja.

Washindi hao walipatikana mara baada ya kununua Omo na kuingia rasmi kwenye droo kubwa inayochezeshwa katika Supermakert kila jumamosi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa Unilever Tanzania, David Minja kwanza aliwapongeza washindi wote haswa watatu waliopatikana katika droo ya mwisho kukamilisha idadi ya washindi kumi na mbili(12) ambao ni Nsalu Mbaga(29yr) mkazi wa Ubungo Riverside aliyeshinda katika Supermaket ya Game Mlimani City, Angel Nyange(23yr) mkazi wa Kimara Mbezi alieshinda katika Supermaket ya Choppies Mlimani City na Mueen Mohamed(59yr) aliyeshinda katika Supermakert ya Shoppers ambao walijishindia pesa taslimu Shilingi milioni moja kila mmoja.

Aidha David Minja aliwaomba pesa walizoshinda wakazielekeze kwenye elimu kwa watoto wao kama kauli mbio ya kampeni inavyo sema “Tusua Ada na Omo”. Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Omo wanatambua kama jamii ya Watanzania imetoka katika kipindi cha Siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya hivyo wakaona ni jambo jema kuungana na wanafamilia katika kipindi hiki cha watoto kwenda shule kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupitia promosheni hii.

Alisema David, katika Promosheni hii ya Tusua Ada na Omo jumla ya Shilingi milioni (7,500 000/=) zimetolewa kwa washindi 9 ikiwa kila mmoja alijishindia pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) na washindi 3 waliopatikana katika droo ya mwisho kila mmoja alijishindia pesa taslimu shilingi milioni moja.

Alisema David ushiriki ulikuwa wazi kwa kila mtu lakini ilipaswa uwe na umri zaidi ya miaka 18, na lazima ununue Omo 1kg moja ziwe pakti mbili au 500gm pakti ziwe nne au 3.5kg pakti moja,ambapo mshiriki alipewa kuponi na kuingizwa kwenye droo iliyochezeshwa kila jumamosi ya juma hilo. Asanteni kwa washiriki wote mliojitokeza kushiriki katika kipindi chote cha Promosheni hii na hongereni sana kwa washindi wote mliobahatika kujishindia zawadi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad