HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 7 February 2019

WAKUU WA SHULE ZA JWTZ WAWEKA MIKAKATI TISA KUBORESHA MATOKEO KIDATO CHA NNE NA SITA

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Wakuu wa Shule zinazomilikiwa na jeshi la ulinzi la wananchi JWTZ wametakiwa  kuboresha uendeshaji wa shule hizo ili kuendana na kasi ya Serikali na kukidhi mahitaji  na mwongozo wa Rais na Amiri Jeshi Mkuu  Dkt John Magufuli kuwa nchi ya uchumi wa kati kwa kuzalisha wahitimu wanaoendana na azimio hilo.

Maagizo hayo yalitolewa na Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita JWTZ  Meja Jenerali Alfred Kapinga wakati wa Kikao na Wakuu hao wa Shule yenye lengo la kutathmini na kuweka maazimio kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi Jijini Dar es Salaam.

Alisema kufanya vizuri kwa shule za Jeshi ni wajibu ambao pia umekuwa ukisisistizwa na mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance mabeyo kutokana na mazingira ya Shule husika.

“ Hatuna sababu kuacha  kujitofautisha na shule za kiraia kutokana na mazingira ya shule zetu ziliko na Walimu katika shule hizo wakiwemo ambao ni wanajeshi hivyo ni matarajio ya Mkuu wa Majeshi kuona Utofauti huo kutokana na wananfunzi wanaohitimu katika shule hizo.” Alisema Meja jenerali Kapinga.

Aliongeza kuwa mwanafunzi anayemaliza katika Shule ya jeshi la Anga Ngerengere na Anayemaliza katika Shule ya Wanamaji Kigamboni na anayemaliza Makongo na shule nyingine Wanatakiwa kuwa tofauti kutokana na Elimu ya Ziada iliyotokana na Fursa ya Uwepo wa shule katika mazingira husika.

Pia aliwataka Kuanzisha Mafunzo ya Ufundi Stadi ili nayo kuwa Sehemu ya Utofauti wa Shule hizo kwa kuzalisha Wataalamu wa kati na wa chini watakaojiajiri lakini pia kuajiriwa katika Viwanda na fani husika.

“ Navy  niliwaelekeza wameanza na wameanza kwa mafanikio sasa kilichobaki ni kuboresha  elimu inayotolewa na chuo ili kuweza pia kujitangaza na kuwa fursa ya kupata Wanafunzi wa Kutosha  na kutoa Mchango stahili kwa Nchi”.  Alisema Mkuu huyo wa Mafunzo na utendaji Kivita.

 Aliongeza kuwa nidhamu ni kitu muhimu hivyo wanafunzi wanaomaliza katika Shule za kijeshi wanatakiwa kuwa na nidhamu zaidi kuliko wanafunzi katika shule nyingine wakiakisi Nidhamu iliyoko katika jeshi ingawa yasiwe mafunzo kama ilivyokuwa kwa Shule ya  Wavulana ya Tabora.

Wakuu hao wa shule za JWTZ wameahidi kufanyia kazi maazimio hayo ikiwa pia ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kurejesha majina ya shule za jeshi  ikiwemo uanzishaji wa vyuo vya ufundi kwa fani zilizokaribu na shule husika

Miongoni mwa maazimio walioweka ni uanzisjhaji masomo ya Sayansi ya Kijeshi, kusimamia ipasavyo walimu,nidhamu, uboreshaji miundombinu uanzishwaji klabu za hesabu,kufufua vipaji kwa shule za michezo na kuboresha mahusiano na wadau wengine wa elimu ili kuendana na mabadiliko.

Pia  Wakuu hao wa Shule wameazimia Kuongeza Ufaulu kwa kuondoa  Divisheni  O  kwa baadhi ya Shule zilizopata matokeo hayo na  Divisheni IV  kwa shule zenye ufaulu wa mwisho wa Divisheni IV kwa wahitimu wa Kidato cha Nne  na Sita na Ufaulu wa chini kubakia Divisheni III.

Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania linamiliki Shule 10 Nchini ambazo ni Nyuki  Unguja , Al Khamis Camp  Pemba, Airwing,  Makongo Jitegemee  na Kigambo zilizoko Dar es salaam, Ruhuwiko Songea,Unyanyembe Tabora, Kawawa Mafinga Iringa  na Kizuka Morogoro.

Uanzishwaji wa shule hizo ulikuwa na  Lengo la kutoa Elimu kwa Askari wake na baadae kutoa Elimu kwa Familia za Askari husika lakini baadae kwa jamii Nzima ambayo imekuwa ikinufaika kwa kiasi kikubwa na Shule hizo
 Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Alfred Kapinga Katikati akizungumza na wakuu wa Shule zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ hawako pichani katika kikao cha Utendaji kuhusu maboresho ya Shule hizo Jijini Dar es Salaaam kulia na Mkurugenzi wa wa Mafunzo na Elimu Brigedia Jenerali Maurius Mhagama. ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Alfred Kapinga Katikati akizungumza na wakuu wa Shule zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika kikao cha Utendaji kuhusu maboresho ya Shule hizo Jijini Dar es Salaaam. ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad