HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 28, 2019

WAAJIRI WANAOKWAMISHA USHUGHULIKIAJI WA RUFAA ZA MASHAURI YA WATUMISHI WA UMMA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU

Watendaji katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka, Sekretarieti za mikoa na Halmashauri za wilaya nchini wametakiwa kutokwamisha jitihada za Tume ya Utumishi wa Umma katika kushughulikia rufaa za mashauri ya watumishi wa umma kwa kutuma vielelezo sahihi vinavyohitajika.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) alipokuwa akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Mhe. Mkuchika amesema kuwa, baadhi ya waajiri na watumishi wa umma wamekuwa wakikaidi au kuchelewa kutekeleza maelekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma ya kuwataka kuwasilisha vielelezo vinavyowezesha ushughulikiaji wa rufaa za mashauri ya watumishi jambo linalokwamisha ushughulikiaji wa rufaa za watumishi.

Amewataka waajiri na watumishi wa umma nchini kutoa ushirikiano wa dhati kwa Tume ya Utumishi wa Umma kila wanapotakiwa kufanya hivyo na kumwagiza Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kuorodhesha waajiri wote watakaoendelea kukaidi maagizo ya Tume ili hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Mhe. Mkuchika amewatahadharisha watumishi na waajiri wanaokwamisha michakato ya ushughulikiaji wa rufaa za watumishi kuwa wanaathiri dhana nzima ya utawala bora na wanakwamisha utoaji wa haki kwa watumishi wa umma na kusisitiza kuwa hatomvumilia mwajiri au mtumishi yeyote anayeharibu heshima yake aliyoijenga kwa miaka mingi.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Rosy Elipenda amemhakikishia Waziri Mkuchika kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa na kuongeza kuwa Tume itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uadilifu bila upendeleo wowote.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bi. Immaculate Ngwale alipowasili Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam kuzungumza na watumishi wa Tume hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi kati yake na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu, Dkt. Stephen Bwana.
 Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Dkt. Stephen Bwana akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa Tume wakati wa kikao kazi kilichofanyika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo.
 Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akitoa neno la utangulizi wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad