HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 28, 2019

DKT NDUGULILE AMEITAKA JAMII KUTOWANYAYAPA WAGOJWA WA RARE DISEASE

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka  wananchi kuacha kunyanyapaa wahanga wa magonjwa ya (rare disease), magonjwa yanayoathiri watu wachache ambayo ni Kuathirika kwa  ubongo,kuathirika kwa misuli inavyofanya kazi,uti wa mgongo na mengine mengi.

Dkt Ndugulile ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam  katika kumbukumbu ya siku ya siku ya Rare disease  duniani kote inayoadhimishwa kila ifikapo februari 28 kila mwaka, ambayo ilianza kuadhimishwa barani Ulaya na kuungwa mkono na nchi nyingi,  ambapo nchini Tanzania ilianza kuadhimishwa rasmi mnamo mwaka 2016.

Dkt Ndugulile amesema kuwa lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kuhamasisha jamii  kuelewa kuhusu magonjwa hayo na athari zake, maana yake ni nini, na kutohusisha magonjwa hayo  na masuala ya kishirikina

Aidha naibu huyo amesema kuwa changamoto katika magonjwa hayo adimu duniani utambuzi wake kwa wakati umekuwa mgumu, matibabu yake pia ni magumu,vile vile matunzo mabovu ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

"Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi tutajadili yale muhimu, na niwapongeze wazazi ambao wanaendelea kusimamia haki za watoto"amesema Dkt Ndugulile.

Vile vile Sharifa Mbarak mzazi wa mtoto Ally ambaye ni mhanga wa magonjwa hayo amesema kuwa mwanae alianza kuumwa akiwa na miaka miwili na nusu lakini hakukata tamaa na matatizo ya mtoto wake,pia amekuwa akifuata ushauri  wa madaktari mpaka sasa alipofikia.

Sharifa amesema kuwa Matatizo hayo ya kupooza mwili yamepelekea Ally asiende shule ikiwa ana ndoto  nyingi sana Kama watoto wengine.

"Kutokana na uzoefu wangu nimepata msukumo na kuamua kujitoa kwa jamii ili wagonjwa walio na magonjwa haya na rai wenye mapenzi mema tujenge uelewa muhimu ili tuweze  kupaza sauti kwa pamoja"amesema bi Sharifa .

Hata hivyo Daktari  mfumo wa ufahamu kwa watoto MUHAS Edward Kija amesema kuwa  takwimu za magonjwa mengi yanayoathiri watu wachache katika 60,000 mmoja ndio ameathirika, na huweza kurithishwa  magonjwa hayo kutoka kwa wazazi wakati mtoto akiwa tumboni kwa mama katika hatua za ukuaji tatizo linapotokea mtoto anaweza akazaliwa na magonjwa hayo.

"Ili kuepuka magonjwa haya katika jamii ni kuhakikisha uelewa wa haya maradhi, kuhakikisha watu wanafahamu dalili za athari pamoja na kuboresha ufahamu na uelewa katika vituo vyetu vya afya"amesema Dkt Kija.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na  wadau mbalimbali leo wakati wa mahadhimisho ya siku ya ( Rare disease)  ni magonjwa mengi ambayo yanawapata watu wachache duniani Jijini Dar es Salaam.
 Sharifa Mbarak mzazi wa mtoto Ally ambaye ni mhanga wa magonjwa hayo akizungumzia leo Jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya rare disease  duniani jinsi ugonjwa huo alivyoupokea kwa kumuuguza mtoto wake ambapo ameonyesha kupambana bila kuchoka
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad