HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 26, 2019

TFF IFIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA

Na Agness  Francis, Blogu ya Jamii
KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  imefunguka rasmi kuwa itatangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu ya Yanga  ifikapo machi 5 mwaka huu. Hiyo ni  baada ya  kamati hiyo kukaa kimya kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo iliyokita maskani yake Jangwani maeneo ya Kariakoo Jijini Dar Da Salaam.

Amesema hayo mwenyekiti wa kamati  ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  Ally Mchunguhela  kuwa tayari ameshakutana na viongozi wa klabu ya Yanga  na kukubaliana  kuwa sasa  kinachosuburiwa ni kutangazwa kwa tarehe rasmi ya uchaguzi huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa klabu hiyo.

Mchungahela amesema kuwa uchaguzi huo ulipaswa kufanyika januari 13 mwaka huu  lakini kutokana na  baadhi ya wanachama wa Yanga kufungua  kesi mahakamani kusimamisha mchakato huo  na kupelekea zoezi zima  la uchaguzi  kusimama.

"Uchaguzi wa Yanga  utafanyika na hakutakuwa tena na mchakato mwingine  mpya  bali utaendelea palepale  ulipokuwa umefikia ,na  ifikapo Tarehe 5 Machi tutatangaza rasmi tarehe  mpya ya uchaguzi wa  Yanga na naamini utafanyika",amesema mchungahela.

Aidha Mchungahela amesema kuwa  mpaka kufikia tarehe itakayotangazwa rasmi ya uchaguzi  huo kila kitu kitakwenda sawa na hakutakuwa tena na kizuizi kingine ambacho kitafanya mchakato mzima kusimama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad