HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 26, 2019

MAFUNZO YA KUNDI LA NNE YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO YAZINDULIWA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wamezindua mafunzo ya kundi la nne  kwa wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa miezi 9 na yatakuwa wanakutana mara 14 ikiwemo na kufanya mtihani na lengo kuu itakuwa ni kulenga zaidi katika kuwapa mwongozo bora wafanyakazi wa kike ili waweze kumudu nafasi zao za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.



Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa wameshasajili wafanyakazi wa kike 31  kutoka makampuni tofauti ambapo wapo waliolipiwa na kampuni zao na wale waliojilipia wenyewe.

Dkt Mlimuka amesema mafunzo haya yatachochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya kampuni na yatawapa ujasiri wanawake kuomba nafasi za uongozi sehemu mbalmbali ikiwemo bodi ya wakurugenzi..

Amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano, kuomba nafasi za juu za uongozi  na katika maisha yao kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kwa muda wa siku 14 muda wa darasani kwa kozi zote  ndani ya miezi tisa na yatafanyika kwa mfumo wa kuunganishwa na shughuli za kila za muhusika mahali pake pa kazi.



" Tumewasajili wahitimu wote kama wafanisi wa bodi za wakurugenzi na uongozi, ujuzi huu utaendelezwa katika kizazi cha baadae lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na mazingira bora ya kazi," amesema.

Amesema kuwa, makampuni mengi yanayoonozwa na wanawake yamekuwa na ufanisi mkubwa sana kwenye maendeleo na yamekuwa na tija na mchango mkubwa na kwa mafunzo haya ya nne kumekuwa na muitikio mkubwa sana.

Dkt Mlimuka aliongeza kuwa ATE inatambua ushiriki kutoka makampuni hayo kama chachu ya kuendeleza mipango mikakati katika usawa, elimu bora na mazingira bora ya kazi katika kuinua uchumi wa nchi.

Kwa upande wa Naibu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB Ester Kitoka amesema kuwa wameamua kudhamini kozi ya nne ya mwanamke wa wakati ujao kwani yamekuwa na umuhimu mkubwa sana katika jamii.

Amesema tafiti zinaonesha kuwa mwanamke ana mchango mkubwa sana katika makampuni na wamekuwa na tija na hicho kimeweza kuwapelekea na kuwaleta wafanyakazi wao wa CRDB kuja kupata mafunzo hayo uweze kuwasaidia katika nafasi nyeti za juu.

Moja ya washiriki wa mafunzo hayo, Mkuu wa Idara wa Rasilimali watu wa Benki ya I & M, Martha Kimweri  amesema, mafunzo haya yanawaleta wanawake pamoja na kubadilishana mawazo, kujifunzam na kuweza kutatua changamoto wanazokutana nazo katika majukumu ya kila siku.


Programu huu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) ilizinduliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu mwaka 2016 ambapo ililenga zaidi kuongeza ufanisi kwa waajiri wa kike mahali pa kazi pamoja na mambo mengine ilibanishiwa kuwa wahusika wataunda mtandao wa kubadilishana uzoefu katika fani mbalimbali.
Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua mafunzo ya awamu ya nne ya wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.

Naibu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB Ester Kitoka akielezea mada katika ufunguzi wa mafunzo ya awamu ya nne  ya wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania. Picha ya chini washiriki wakiwa wanasikiliza makini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad