HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 11 February 2019

RC NDIKILO AWAGEUKIA WAFUGAJI MAGINDU

 NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemuagiza mkuu wa kituo cha polisi Mlandizi, ofisa tarafa na watendaji wa kata ya Magindu kuwakamata wafugaji kumi wanaodaiwa kuingiza mifugo yao kwenye mazao ya wakulima na kuwasababishia hasara pasipo kuchukuliwa hatua za kisheria tangu mwaka 2016.

Aidha ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Kibaha, kuweka upya mpango wa matumizi bora ya ardhi,  katika kijiji cha Magindu, Lukenge na Mizuguni ili kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji. Akitoa maagizo hayo, wakati akizungumza na wakazi wa Magindu, katika ziara yake, Ndikilo alisema wafugaji wasipewe kichwa kutokana na uwezo wao ili kukandamiza wakulima. 
"Hii ni mara ya mwisho, nipo serious ,sifanyi mzaha, wasimamieni kikamilifu wafugaji hawa, wanalisha mifugo yao usiku katika mashamba ya watu, wanatamba Magindu ,Ni lazima haki itendeke, pasipo kukandamiza walio wanyonge"alisisitiza Ndikilo. Mkuu huyo wa mkoa aliwaasa ,wakulima na wafugaji kila mmoja kumheshimu mwenzake ili kuishi kwa amani na upendo. 

Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi wa migogoro ya wakulima na wafugaji Magindu, Iddi Ngozoma alibainisha, tangu kamati iundwe miaka mitatu sasa ,mkulima hajawahi kushinda kesi hivyo,  wananchi hawana imani na utendaji kazi wa mahakama ya mwanzo Magindu. Akitolea ufafanuzi suala hilo, mkuu wa idara ya ardhi na maliasili wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Greison Gozibath alisema, kijiji cha Magindu kilipimwa 2007 ,pia kilifanyiwa matumizi bora ya ardhi 2010.

Alieleza, wakati huo kijiji cha Mizuguni hakikuwepo ambapo kilizaliwa 2013-2014. Gozibath alibainisha, kwasasa inatakiwa kufanya mpango huo kwa vijiji vyote na wanatarajia kuviingiza katika matumizi bora ya ardhi kwenye bajeti 2019-2020. Hata hivyo, utekelezaji huo utawataka wananchi kugharamia kulingana na kijiji husika ambapo gharama huanzia sh. milioni 12 hadi milioni 15-18.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad