HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 11, 2019

MAKAMBAKO YAZIDHATITI KUMLINDA MTOTO DHIDI YA VITENDO VYA KIKATILI

Halmashauri ya Mji wa Makambako imejidhatiti katika kuhakikisha wanamlinda mtoto na vitendo vyote vya kikatili dhidhi yake vinavyokatisha ndoto zake vimewemo mimba na ndoa za utotoni, utekaji na mauaji ya watoto.

Hayo yamebainika leo katika kikao kazi cha Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto ya Halmashauri ya Makambako ilipokutana mjini hapo kujadiliana namna bora ya kuondoka na vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Bw.Paul Malala amesema imejiwekea Mikakati kwa kutoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji na mitaa kuhakikisha watoto wanalindwa ipasavyo.

Ameongeza kuwa watendaji wa Kata na Vijiji wamepewa maelekezo kuhakikisha wanafuatiliwa wale wote wanaowafanyia vitendo vya kikatili na taarifa zao kufika sehemu husika.

“Tutahakikisha kwamba mtoto na mwanamke analindwa watendaji wa vijiji na mitaa wahakikishe watoto na wanawake wanalindwa ipasavyo” alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu amesema kuwa lengo la wataalam hao kuja katika Mji wa Makambako ni kushirikiana na Wataalam wa mji huo kupanga mpango mkakati bora wa ndani ya kuondoka na na vitendo vya ukatili dhoidi ya wanawake na watoto.

Amesema  kikubwa Kamati ya Ulinzi dhidi ya Maanamke na Mtoto inawajibu wa kutoa elimu kwa  wanajamii kuhusiana na malezi namatunzo kwa mtoto na kumlinda dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto katika maeneo yao.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuwa Kamati hizo zina majukumu makubwa ya kuhakikisha mtoto na mwanamke analindwa katika kuweka mikakti ya kuwalinda watoto na kuhakikisha wahanga wa vitendo vya ukatili wanapata huduma stahiki na kwa wakati.

 Aidha akielezea kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Mtoto namba 21 ya Mwaka 2009, Mwanasheria kutoka Wizaraya Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Denis Bashaka amesema kuwa  Sheria ya Mtoto inatoa adhabu kali kwa wale watakahusika na kumfanyia vitendo vya ukatili Mtoto.

Ameongeza kuwa vitendo vingi kwa mkoa wa Njombe vinaushishwa na imani za kishirikiana ila bado vitendo hivyo ni kinyume cha Sheria ya Uchawi Sura 18 2002 inakataza upigaji wa ramli ambapo waganga wengi wa Jadi wamekuwa wakiusishwa katika kupiga ramli ambazo ni chonganishi zinazopelekea mfarakano katika jamii.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Bw.Paul Malala akizungumza na Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto pampja na Halmashauri ya Mji huo katika  kazi kilichowakutanisha kujadili namna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu akieleza lengo la ujio wa Wataalam hao katika kikao kazi kilichowakutanisha kujadili namna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Mwanaisha Moyo akileza umuhimu wa Kamati ya Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto katika kusaidia ulinzi na usalama kwao katika kikao kazi kilichowakutanisha kujadili nnamna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Denis Bashaka akieleza namana Sheri ya Mtoto na ya Mwaka 2009 inavyomlinda Mtoto wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha kujadilia nnamna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya MWanamke na Mtoto ya Halmashauri ya Mji wa Makambako wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao kazi kilichowakutanisha kujadilia nnamna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad