HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 26, 2019

MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI SHINYANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Shinyanga tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 5. Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa njia ya barabara akitokea mkoani Tabora ambapo napo alikuwa na ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo.

Mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga Makamu wa Rais alitembelea kituo cha Afya cha Samuye na kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. “Serikali ina kila nia ya kusogeza huduma za afya bora kwa wananchi”alisema Makamu wa Rais.

Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inakuja na sheria ya mpango wa bima za afya kwa wote ambayo itamuhitaji kila mtanzania kuwa na bima ya afya. Makamu wa Rais amewataka wakazi wa kata ya Samuye kushirikiana katika kuzuia mimba za utotoni kwani kwa kiasi kikubwa zinahatarisha maisha ya watoto wa kike.

Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara amesisitiza Halmashuri kutenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuzitaka halmashauri zote kumalizia maboma ya zahanati wakati serikali kuu inaleta pesa za kumalizia maboma ya shule na madawati.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa kata ya Tinde waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili mkoani Shinyanga akitokea mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Samuye mara baada ya kutembelea na kukagua  kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad