BENKI YA CRDB YAJIPAMBANUA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI YA KUTOA ELIMU BURE NA BORA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 26 February 2019

BENKI YA CRDB YAJIPAMBANUA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI YA KUTOA ELIMU BURE NA BORA

Benki ya CRDB imeendelea kujipambanua kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufili ya kutoa elimu bure na bora kwa wanafunzi wote nchini. Hilo limedhihilika leo Februari 26, 2019 kwa kukabidhi madarasa mawili pamoja na madawati 40 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 60 kwa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls).
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kulia), Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Neema Mori (wa pili kushoto) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakingukua kitambaa cha jiwe la msingi wakati wa ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa msaada wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Neema Mori akizungumza machache katika ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifurahi jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati akisalimia wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.

1 comment:

Post Bottom Ad